.

ROSE NDAUKA MFANO WA KUIGWA KWA WASANII--AAMUA KUFANYA USAFI WA JIJI LEO,WASANII WENZAKE WAMUUNGA MKONO

Msanii wa fiklamu tanznia rose ndauka akiwaongoza wasanii wenzake kufannya usafi wa kujitolea leo jijini dar es salaam eneo la mnazi mmoja
         MSANII wa Bongo muvi Rose Ndauka kwa kushirikiana na Wasanii  wenzake wa Bongo muvi leo wamefanya kitu  cha Tofauti na kuwaacha wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam midomo wazi.
        
 Mshangao huo kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam umejitokeza leo Wakati Wasanii hao walipokuwa wanafanya usafi wa kufagia barabara kwenye Barabara ya Mnazi Mmoja jijini hapa hadi mtaa wa Lumumba na kufanya Watu waanze kushangaa.
Akizungumzia  Maamuzi hayo ya kufanya usafi katika jijiji hili, Msanii wa Bongo Muvi, Rose Ndauka alisema wameamua kufanya usafi ikiwa ni mfano kwa wananchi wa Dar Es Salaam kuwafanya waweke Mazingira yao Masafi.
       
     “Tumeamua kufanya kazi ya kufanya usafi leo katika ,mkoa huu ni sehemu ya kuonyesha umma wa Watanzania,Lazima tuyaweke Mazingira yetu Masafi na kufanya watu wayapende,Na leo nyie wandishi wa Habari mmekuwa mashahidi mmeona kazi kubwa tuliyofanya leo kwa kushirikiana na wasanii wenazangu”
    
       “Natumia Fursa hii kuwapongeza sana Wasanii wenzangu wa Bongo Muvi waliojitokeza na kujumuika kufanya Usafi katika jiji hili vilevile nampongeza Meya wa Halmashauri ya ILala Jery Slaa na Mkurungenzi wa Halmashauri ya ilala pamoja na Viongozi wote wa Mkoa huu waliotupa hamasa ya kufanya hivi leo”Alisema Ndauka
       Rose Ndauka Ambayeni Miongoni mwa Wasanii Bora kwa sasa katika Tasnia ya Filamu nchini Tanzania na Afrika Mashariki na Kati aliiomba Serikali kuwaongezea Vifaa vya kufanyia kazi watu wanaofanya kazi ya Ufagiaji Barabarani kwani vifaa ni vichache sana na vinapelekea jiji kuwa chafu.

       Kwa Upande wake Meya wa Manispaa ya Ilala Jery Slaa alimpongeza sana Rose Ndauka na Wasanii wengine wa Filamu hapa nchini waliokuwa Tayari kujumuika na Rose katika Suala la Usafi na kusema ni Jambo la Kumpongeza na la kuigwa kwa watu wengine wenye mapenzi mema na nchi hii kama Ndauka.
      
      Vilevile kwa Upande wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSPF ambao ndio walidhamini shuhuli nzima na kufanikisha zoezi hilo la usafi nao walisema wao kama mfuko wa Jamii hawataacha kuweka nguvu katika mambo muhimu kama aliyofanya Ndauka,kwani yana tija katika taifa letu Changa,ikizingatiwa usafi ni njia ya kupunguza Magonjwa ya Mlipuko

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.