.

LIGI KUU TANZANIA,MTIBWA YAIONGEZEA MACHUNGU YANGA MUDA HUU

Kikosi cha sasa cha Mtibwa FC kilicho kabiliana na changamoto ya kuvunja kibuyu cha kutofungwa mechi hata moja Uwanja wa Jamhuri mbele ya Yanga  kwa miaka mitano sasa
 YANGA SC haijashinda mechi Uwanja wa Jamhuri Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar kwa miaka mitano sasa na leo imeshuka kwenye Uwanja huo kumenyana na Wakata Miwa hawa wa Manungu.
Septemba 19 mwaka 2009 ndipo Yanga SC iliposhinda kwa mara ya mwisho Uwanja wa Jamhuri wakati huo ikiwa chini ya kocha Mserbia, Profesa Dusan Savo Kondic na tangu hapo kila inapokwenda huko matokeo mazuri kwao yamekuwa sare.
Wachezaji wa mwisho kuipa Yanga SC ushindi Uwanja wa 
Jamhuri dhidi ya Mtibwa walikuwa ni Nurdin Bakari aliyefunga dakika ya 55 na Mrisho Ngassa dakika ya 57, lakini zaidi ya hapo mechi zilizofuata Wana Jangwani hao ama wamefungwa, au kutoa sare. 
mpaka Msike corner inatoka uwanjani leo hakuna timu iliyo fanikiwa kuona lango la mwenzake uku yanga ikiwa nafasi ya pili kwa kuwa na point 39 huku mtiwa wakiwa na point 26.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.