manaja mawasiliano wa kampuni ya tigo tanzania akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini dar es salaam
Tigo Tanzania imetangaza
kushirikiana na taasisi ya usalama wa pikipiki nchini katika kuzindua Mpango wa
Huduma Salama ya Usafiri wa Bodaboda Kitaifa itakayofanyika mjini Dodoma, 23
Machi, 2014.
Akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, iliyowashirikisha pia wakala
wa usalama wa pikipiki nchini (TAMOSA), Meneja Mawasiliano wa Tigo, John
Wanyancha, alisema kwamba udhaminiwa Tigo katika mpango huo wakitaifa wa usalama
wa bodaboda nchini ni ishara ya kwamba kampuni hiyo ya simu inajali na kufuatilia kwa karibu kuhusu masuala ya usalama
barabarani nchini.
“Wote ni mashuhuda
wajinsi biashara hii ya pikipiki ilivyoweza kushamiri ndani ya muda mfupi nchini.
Kupitia bodaboda na bajaji vijana wetu wameweza kujiajiri wenyewe na kuweza kujipatia
kipato kinacho wasaidia kumudu maisha,”alisema Wanyancha.
“Lakini kila kitu
huja na changamoto zake, na katika hili suala la ajali barabarani limekuwa dosari
kubwa. Kama kampuni, tuliamini kwamba hii itakuwa fursa nzuri kwa sisi kama wadau
kujaribu kuhamasisha kuhusu usalama barabarani kwa ajili ya kusaidia kupunguza idadi
ya ajali zinazotokea huku tukihakikisha kwamba sekta hii inaendelea kuwa chachu
ya ajira kwa vijana nchini,”alisema.
|
No comments:
Post a Comment