Na karol vicent
SIRI za kushindwa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwenye chaguzi mbalimbali yabainika,na kama
chama hicho isipotafuta ufumbuzi wa siri hiyo basi kisubili miujiza kwenye
uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Huku ikiwa ni siku moja imepita
Baada ya Kumalizika Uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kalenga na Chama
cha Mapinduzi CCM kuibuka mshindi na kuigalagaza vibaya sana Chama cha
Demokrasia na Maendereo CHADEMA,
Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa
Mtandao huu umebaini udhaifu wa Kusimamia misimamo yao wanayoitoa kwa
viongozi wa Juu wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe na Katibu
Dokta Slaa ni miongoni za sababu chama hicho kufanya vibaya na kuendelea
kufanya Vibaya kwenye chaguzi mbalimbali zinazokuja ikiwemo wa Serikali za
Mitaa.
Sababu kubwa iliyogundulika inakitafuana chama hicho ni Idadi ndogo
ya Vijana wenye umri wa miaka 18 ambao ni hazina kubwa ya Chama hicho
kutoandikishwa kwenye Daftari la kupiga kura na hata wale walioandikisha nao
wamepoteza Shahada za kupiga kura.
Duru hizo zinasema kwa mujibu wa
tafiti mbalimbali zinaonyesha vijana Takribani Milioni kumi waliofikisha umri
wa kupiga kura kisheria hawajaandikishwa kwenye Daftari hilo huku wengine
waliojiandikisha teyari wamekufa huku taarifa zao hazijafika katika Tume hiyo ya
uchaguzi.
Kwa Mujibu wa tume ya Uchaguzi
nchini wamesema wao hawana Fedha za kuboresha Daftari hilo,huku ikumbukwe mara
ya mwisho Daftari lilifanyiwa marekebisho mwaka 2009 na mpaka sasa miaka mitano
imepita huku bado alijafanyiwa marekebisho.
Kile kinachotafsriwa na wengi
uwenda uwezo mdogo wa viongozi hao Juu wa Chama hicho, katika kusimamia
misimamo wanayoyasema,ama viongozi hao wanakuwa wanataka umaharufu
wakisiasa kwa wanachama wao.
Ikumbukwe Mwenyekiti wa Chama hicho
Freeman Mbowe katika mkutano wake na waandishi wa Habari uliofanyika miezi
miwili iliyopita aliutangazi Umma wa Tanzania Chama hicho hakitashiriki
Uchaguzi wowote Mpaka Daftari la kudumu la kupiga kura litakapoboreshwa.
Mbowe, ambaye ni Mbunge wa Jimbo
la Hai na vilevile kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni alizidi kusema
wao chadema wamebaini Vijana zaidi ya milioni Nane hawana kadi za kupigia huku
tayari wamefikisha umri wa miaka 18 na wengine wamepoteza kadi zao na kuipa
onyo kali tume ya Uchaguzu nchini kuboresha Daftali lasivyo chama hicho
akitashiriki chaguzi zozote za nchi hii.
Lakini viongozi hao kuonyesha
ugeugeu kwa wanachama wao katika kusimamia misimamo wanayoitoa , Hivi leo Chama
hicho Kiendelea kushiriki kwenye Chaguzi mbalimbali hapa nchini huku kikijua
kabisa hazina yao kubwa ni vijana ambao hawana Kadi za kupigia kura na huku
chama cha Mapinduzi CCM kikitumia nguvu kubwa ya Wanachamma wazee hukuwakijua
wanachama wengi wa Chadema ni Vijana kutilia fitina kwenye Tume ya Uchaguzi
nchini.
Chadema ambacho ndicho chama Kikuu
cha upinzani Nchini,ni Dhahiri viongozi wake ni wababaishaji kwa wananchama
wake ndio maana wanashindwa kusimamia matamshi wanayoyatoa,
Swali la kujiuliza Viongozi wa
Chadema mpaka wanaingia kwenye uchaguzi wa Kalenga walikuwa hawafahamu kuhusu
hoja ya Daftari la kupiga kura? Je iko wapi misimamo ya Mwenyekiti wa Chadema
kwamba watasusia Uchaguzi mpaka Daftali la wapiga kura litakapoboreshwa?
Mbowe na Katibu wake Dokta Slaa
walikuwa wanawadanganya Wananchi au tuanze kutilia Shaka viongozi hao walipewa
kitu kidogo na Tume ya Uchaguzi mpaka wakaingia kwenye uchaguzi wa Kalenga?
Na leo hii Tayari Chama hicho
kimethibitisha Kushiriki kwenye Uchaguzi wa Jimbo la Chalinze Je kunahaja Gani
chama hicho kushiriki kwenye uchaguzi huo huku kikijua hakina wanachama
wakuweza kuwasaidia kushinda uchaguzi huo?
Au, Dhana ijengeke viongozi Hao wanapenda kuteketeza pesa kwenye Kampeni
kwa kutumia Chopa angani huku wakijua kabisa hawana wanachama wakuwapa Dola,Chadema
kina viongozi wakutoa matamko na kuwa na nyuso za kujiamini kutoa matamko
pasipo kusimamia misimamo yao.
Tukitoa uchaguzi wa Chalinze
kunaujaguzi wa Serikali za mitaa Je kwa mfumo huu wa Daftali la wapiga kura
kutoboreshwa na kuwapa Fursa wananchi kusajiliwa je chama hicho kitegemee
kushinda kwenye uchaguzi huo.
Kwa Tafsiri hii Uchaguzi wa Mdogo wa
madiwani pamoja na Jimbo la Kalenga ingekuwa Ndoto kwa chama hicho kushinda
kutokana na idadi ndogo ya wanachama.
Wanachama wa Chadema wanahaja ya
kuwaangaliwa Viongozi wao wa Juu kwa makini sana wasiwabeze watu wanaowapinga
viongozi hao wa juu kwakuwa wanahoja ya kuwapinga kwakuwa
wamekuwa ni watu wa porojo tuu na sasa wananchi wameanza kuzichoka porojo
zao na kuanza kuwasulubu kwenye chaguzi mbalimbali.
Tafakari,
No comments:
Post a Comment