Wednesday, March 19, 2014

TIGO YATOA MISAADA YA ELIMU KATIKA SHULE YA KILIMANI JIJINI DAR ES SALAAM

meneja wa huduma za kijamii kutoka tigo WOINDE SHISAEL akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya msingi kilimani iliyopo manispaa ya kinondoni jijini dar es salaam ambapo Tigo ilikabidhi msaada wa vitabu 905 vyenye thamani ya milioni 6.1 na tenki la kuhifadhia maji la lita 4000 kwa shule hiyo.


            Katika jitahada za kusaidia kuboresha hali ya maisha ya watanzania kupitia kuwekeza katika mipango ya maendeleo ya kijamii, Tigo Tanzania leo imetoa msaada wa vitabu vya wanafunz iwadarasa la nne hadi la saba vyenye thamani ya shilingi milioni 6.1/- kwa shule ya msingi Kilimani iliyopo jijini Dar es Salaam.
 
tunafurahia


               Akikabidhi msaada huo katika shule hiyo, Meneja wa Huduma za Kijamii kutokaTigo, Woinde Shisael, alisema kwamba kampuni hiyo ya simu inatambua fika umuhimu wa elimu kama kiungo muhimu katika kuchangia mabadiliko kwenye jamii na taifa kwa ujumla.


Wanafunzi wa darasa la nne na la saba wa shule ya msingi Kilimani wakiimba wimbo wa "Tanzania, Tanzania" kama ishara ya uzalendo na kutambua mchango wa Tigo kama kitendo cha kiungwana kwa shule hiyo.


3. Mwalimu Mkuu wa shule ya Kilimani iliyopo Manzese Bi. Zubeda Jeni (kushoto) akimshukuru Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Woinde Shisael kwa msaada wa tenki la kuhifadhia maji la lita 4000 yenye thamani ya Tsh 653,000/- pesa iliyochangishwa na wafanyakazi wa Tigo.
baadhi ya vitabu ambavyo tigo wametoa kama msaada wa shule hiyo

sim tank ambalo tigo wametoa kama msaada katika shule hiyo ya kilimani
            Woinde pia alikabidhi, tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita 4,000 zamaji la thamani ya shilling 653,000/-, pesa iliyokusanywa kutoka kwa wafanyakazi wa Tigo. Alisema msaada huo utachangia kuboresha mazingira bora yakujifunza na kufundisha kwa wanafunzi na walimu shuleni hapo.

No comments: