Tuesday, April 29, 2014

DILI LIMEKAMILIKA! DIDIER KAVUMBAGU AMWAGA WINO AZAM FC

kavumbagu3                       Na Baraka Mpenja , Dar es salaam

 DIDIER Kavumbagu kwaheri Yanga. Hii ni baada ya mchana wa leo kusaini mkataba wa mwaka mmoja na mabingwa wapya wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Azam fc.

 Taarifa hii imethibitishwa na meneja wa Azam fc, wana Lambalamba, Jemedari Said.

“Kavumbagu tumemalizana nae na amesaini rasmi mkataba wa mwaka mmoja, so tutakuwa nae msimu ujao kwenye kampeni ya kutetea ubingwa wetu pamoja na michuano ya klabu bingwa ya Afrika,” alifunguka Jemedari
kavumbangu na nassor
   Mshambuliaji huyo hatari na nahodha wa timu ya Taifa ya Burundi ameamua kumwaga wino Azam baada ya Uongozi wa Yanga kusuasua kumpa mkataba mwingine baada ya ule wa miaka miwili kumalizika.

No comments: