Sunday, April 30, 2017

DC Mjema: Daladala, bajaji zisizokuwa na 'dustbin' kutozwa faini

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewaagiza madereva wa daladala na bajaji kuhakikisha vyombo vyao vya usafiri vinakuwa na kikapu cha kuwekea taka, vinginevyo watatozwa faini ya uchafuzi wa mazingira.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika kufanya kwa vitendo kampeni ya usafi ya kila jumamosi ya mwisho wa mwezi DC Mjema alitembelea kituo cha daladala cha stesheni na kukuta magari mengi ya abiria hayana vikapo vya taka, ambapo wameyatoza takribani magari saba  kiasi cha shilingi 50000 kwa kila moja katika eneo hilo.
Huku kwa upande wa madereva wa bajaji wanaopaki eneo la Soko la Samaki Feri wamepewa onyo na kuombwa kufanya hivyo mara moja kabla hawajachuliwa hatua na mamlaka husika ya Halmashauri hiyo ya Ilala.
Katika hatua nyingine DC Mjema amewataka wafanyabishara wadogo wanaopanga bidhaa zao kandokando ya barabara iliyopo jirani na soko la samaki Feri kujiandikisha kwa afisa mtendaji na kuondoka eneo hilo mara moja, huku Halmashauri hiyo itawapangia maeneo ya biashara ndani ya soko hilo la samaki la Feri.

No comments: