Friday, April 25, 2014

HABARI MPYA---JUKWAA LA KATIBA LAJITOSA MGOGORO WA BUNGE MAALUM,WATANGAZA KUWASULUHISHA,JAJI BARNABAS,NA PATRICE LUMUMBA WAITWA,JUKATA WASEMA HAKUNA KATIBA MPYA MWAKA HUU

Mwenyekiti wa jukwaa la katiba tanzania DEUS KIBAMBA
Na Exaud mtei
Jukwaa la katiba Tanzania JUKATA limejitolea kuratibu maridhiano  miongoni mwa makundi ya kisiasa  asasi za kiraia asasi za wananchi na taasisi zote za muhimu zilizoguswa na migogoro inayoendelea katika bunge maalum la katiba tanzania

     Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za jukwaa la katiba sinza jijini dare s salam mwenyekiti wa jukwaa la katiba bw DEUS KIBAMBA  juu ya tathimini walizozifanya katika bunge hilo wameamua kujitolea kufanya maridhiano hayo kwa kuwashirikisha viongozi maarufu afrika ya mashariki  akiwemo mheshimiwa jaji mkuu mstaafu wa Tanzania BARNABAS SAMATTA ambaye atakuwa mkuu wa jopo hilo la usuluhisho  nandugu  PATRICE LUMUMBA   kutoka Kenya ambaye atakuwa msaidiz
           
       Aidha jukwaa hilo limeonyesha masikitiko yake kwa kile walichookiita ni uvunjifu wa kanuni mara baada ya wabunge zaidi ya mia mbili kutoka nje lakini wabunge waliobakia kuendelea kurekebisha kanuni za bunge hilo jambo ambalo wamesema kuwa haikustaili kwani wana uwezo wa kujitungia sheria.

       KIBAMBA amesema kuwa kutokana na mwenendo wa bunge hilo hadi hapa lilipofikia wabunge hao hawana nia ya dhati ya kulipatia taifa katiba mpya huku akitolea mfano kuwa katiba mpya ilipangwa kuwekwa  saini na Rais siku ya tarehe 26 mwezi huu  yani kesho lakini hadi sasa hata majadiliano ya sura mbili hayajamalizika, na kuwahakikishia watanzania kuwa hakuna katiba mpya itakayopatikana kwa mwaka huu.

             Hata hivyo mwenyekiti huyo amewataka wajumbe wote na asasi zote zilizopo nje ya muendelezo wa bunge hilo maalumu la katiba kuwa tayari kwa maridhiano kwa mtu au taasisi yoyote atakayekuwa tayari kutatua migogoro yao ili kuwezesha upatikanaji wa katiba kwa taifa letu

No comments: