.

HII NDIO HABARI ILIYOTIKISA JIJI LEO---KAULI YA WAZIRI LUKUVI YALETA MAKUBWA,JUMUIYA YA WAISLAAM YAJITOKEZA LEO YATOA TAMKO KALI,SOMA WALICHOKISEMA

Msemaji wa taasisi za Kiislaam Tanzania RAJABU KATIMBA akizungumza na wanahabari mapema leo jijini dar es salaam
Na Karoli Vinsent
KAULI ya uchochezi na kuligawa Taifa kidini aliyoitoa  kanisa, Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri mkuu(sera,uratibu na Bunge) William Lukuvi.Sasa Yazidi kuibuwa Makubwa.

Hivi leo Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, wameandaa kongamano kubwa ili kumshinikiza, Rais Jakaya Kikwete amfukuze kazi,Waziri Lukuvi katika nafasi hiyo,kwa kile wanachokidai analigawa Taifa kidini na kuleta machafuko.


Hayo yalisemwa Leo, na Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini Rajabu Katimba wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo alisema wamefikia maamuzi hayo kuandaa kongamano hilo kutokana na kauli ya kichochezi aliyoitoa waziri huyo.

“Sisi hatukutalajia Waziri mwenye mamlaka makubwa na aliyeaminiwa na Rais na kumwakilisha waziri mkuu kutamka kauli chafu na za uchochezi tena kanisani dhidi ya waislamu nataasisi ya kiislamu iliyosajiliwa kihalali”

“kauli hizi zina nia ya kuletea chuki,kuwatia woga wananchi na hatimaye kuchafua Amani ya nchi na Tumeandaa kuongamano hili kumshinikiza Rais amwajibishe waziri Lukuvi”Alisema  Katimba

Katimba,alizidi kusema wao wanashangaa kimya cha Serikali kumwacha waziri huyo akifanya uchochezi na kuligawa taifa.

“Tunashangaa mpaka sasa viongozi wa Serikali wamekaa kimya na kumwacha Waziri lukuvi akifanya uchochezi,Je maneno yaliyotamkwa na Sheikh Ponda kuhusu mfumo wa  Kristo dhidi ya Waislam yanalingana na haya mh Lukuvi ya chuki na uchochezi”

“Kwa mwenendo huo wa Mh Lukuvi,kwa nini Waislamu na wapenda Amani wote tusiamini kuwa kuna mpango wa Siri kuongamiza Viongozi wa Kiislamu na kuhalalisha mauaji hayo kwa Propaganda na Uchochezi wa Mh Lukuvi?”alihoji Katimba

Kitimba,aliwataka viongozi wa Dini zote kuungana na Kujitokeza kwenye Kongamano la Amani la litakalofanyika tarehe 27 mwezi huu kwenye Makao makuu ya Taasisi hiyo iliyopo Kinondoni Jijini Dar Es Salaam ili Kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete amwajibishe Waziri Lukuvi,na Kujadiri hatma ya Katiba.

Ikumbukwe kauli hiyo ya uchochezi aliitoa Waziri Lukuvi alipokuwa anamwakilisha Waziri Mkuu,kwenye kanisa la Methodist jimbo la Dodomo wakati wa Sherehe za kumtawaza mchungaji Joseph Bundala kuwa Askofu,ambapo Waziri lukuvi alitamka wazi wazi kwamba Serikali Tatu zikipita eti nchi haitotawalika na kuchukiliwa na Jeshi na vilevile makanisa yote nchini yatafungwa na kwamba nchi itakosa Amani.

Lukuvi ambaye ni mbunge wa jimbo la Isimani mkoani Iringa kupitia Chama cha Mapinduzi CCM,alizidi kuongeza kwamba Wanzazibari wanataka kujitenga hili kujitangazia nchi  ya Kiislam.


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.