Thursday, April 17, 2014

KUELEKEA PASAKA--FAN CITY YAJIPANGA KUTOA BURUDANI YA KIPEKEE KWA WATANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Green Stars Industry inayomiliki eneo la FAN CITY Bw. Hasan Rizvi akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mashine za michezo mbali mbali itakayotolewa kipindi cha sikukuu ya Pasaka wakati wa mkutano alioufanya katika eneo la Fun City Kigamboni jijini Dar es Salaam. Pia aliongeza kuwa kwa sasa kampuni yake imeeongeza mitambo yenye uwezo wa kutengeneza mawimbi ya aina sita tofauti kwenye bwawa kubwa la kuogelea


Mkurugenzi Mtendaji wa Fan City, Bw. Hasan Rizvi akionyesha vigari vya mchezo
Moja ya Bwawa la kuongelea

Mawimbi yanayotengenezwa kwa mitambo ya kisasa katika bwawa kubwa la kuogelea lililopo hapa Fun City
Wakati Watanzania wakiwa kwenye maandalizi ya sikukuu ya Pasaka kampuni ya Green Stars Industry inayomiliki eneo la FAN CITY limeongeza mitambo yenye uwezo wa kutengeneza mawimbi ya aina sita tofauti kwenye bwawa kubwa la kuogelea.Mtambo huo wa aina yake utaongeza hamasa kwa waogeleaji kuhisi kama wapo baharin

Akizungumzia mtambo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Fan City, Bw. Hasan Rizvi amesema, lengo la kuoberesha michezo hiyo ni kuwawezesha watanzania kufurahia michezo hiyo pamoja na familia zao wakati huu wa Pasaka.Fun City imekuwa ikitoa burudani safi ya michezo mbalimbali kwa familia na katika kipindi hiki cha Pasaka imeandaa michezo kama Sarakasi, Mazingaombwe na zawadi kemkem kwa watakaotembelea eneo hilo

No comments: