.

MAJAMBAZI WAVAMIA OFISI ZA GAZETI LA MAJIRA,WAKOMBA KOMPYUTA ZOTE

Na Karoli Vinsent
      
          Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa Majambazi wamevamia  makau makuu ya ofisi za Gazeti la majira,zilizopo Jijini Dar Es Salaam na Kuiba Kompyuta zilizopo kwenye Chumba cha Habari.
        
         Kwa Mujibu wa Waandishi wa Gazeti hilo waliozungumza na Mwandishi wa Mtandao huu ambao hawakutaka kutajwa Majina yao kwenye Mtandao huu wakisema wao sio wasemaji wa Gazeti hilo,walithibitisha wezi kulivamia Gazeti hilo na kuiba vitu vyenye Thamani isiojulikana.

   
       “Hizo taarifa ni za Kweli Mana mimi nimefika leo Ofisini nimekuta Kumpyuta zaidi Ya tisa zilizokuwa kwenye chumba cha Habari azipo na zimeibiwa,ambazo tulikuwa tunazitumia kuandikia habari na mpaka sasa ofisi kwetu zimebaki kompyuta nne tu, na sijui sisi wengine waandishi, hizi habari tutaziandika kupitia kwenye nini?”Alihoji mwandishi huyo wa Majira.

     Vilevile Chanzo Kingine cha Habari ambacho kilichopo ndani ya Majira  alisema watu hao walivamia katika ofisi za Gazeti hilo usiku wa kuamkia Leo na kuvunja Juu ya paa la juu na kuingia ndani na kufanikiwa kuiba vitu hivyo.
Mwandishi wa Mtandao huu alimtafuta  Kiongozi wa Gazeti hilo aliyefamika kwa Jina moja la Kagua ili kuzungumia Taarifa hizi.

        “Ndugu mwandishi mimi sijazisikia hizo Taarifa,maana nipo safarini,watafute watu walioko ofisini ndio wanataarifa zote”alisema Kaguo
Juhudi za kumtafuta viongozi wa gazeti hilo zinazidi kuendelea.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.