Wednesday, April 30, 2014

SERIKALI YAENDELEA KUTOA ONYO KALI KWA GAZETI LA MAWIO,SASA WAWATAKA KUFWATA MAAGIZO YALIYOTOLEWA,LA SIVYO----

Na Karoli Vinsent
        
      MKURUGENZI wa Idara ya Habari MAELEZO amelitaka Gazeti la Mawio kufuata maagizo aliyatoa ,Lasivyo wakiendelea kukaidi Basi wasubili hatua kali zaidi.
        
       Kauli  hiyo ya mkurugenzi wa idara hiyo Asah Mwambene,imekuja siku chache kupita baada ya Gazeti la mawio kwa kupitia mkurugenzi wake kusema kwamba hawajapata barua kutoka kwenye Idara hiyo ya Habari maelezo iliyowataka waombe Radhi na kusema hawana barua hiyo ili wao waweze kuchukua  hatua  hiyo wanayoitaka.
          

    Hivi Leo naye mkurugenzi na Idara  ya Habari MAELEZO Assah Mwambene wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, amesema mkurugenzi huyo wa Gazeti hilo ni muongo kwani wao walipeleka Barua hapo ofisi za Gazeti hilo.
    
    “Kwanza niseme huyo kiongozi wa hilo gazeti ni muongo kwani sisi Serikali tumepeleka kabisa Barua kwenye ofisi wa Gazeti hilo na kila tuliomkuta pale alikataa kuchukua barua kwaanzia wafanyakazi wa Gazeti hilo hadi Majirani,sasa huyo anayesema ajapata barua yetu anamaana gani”
  
      “Na sisi tutajua hatua za kuchukua kwenye Gazeti hilo kutokana na kitendo chake cha kudharau na subirini hatua tutakaochukua”alisema Mwambene
  
      Mvutano,huu wa Mwambene na Wamiliki wa Gazeti la Mawio umeibuka siku chache kupita baada ya mkurugenzi wa Idara hiyo kulitaka gazezi hili mawio kuomba Radhi kutokana na Habari aliyoita ni ya Kichochezi.
Wakati wa mkutano uliopita,Assah Mwambene alisema gazeti hilo la wiki linatakiwa kujieleza ndani ya siku tatu.

     Alisema mbali na kujieleza, gazeti hilo limepewa siku saba hadi Aprili 23, mwaka huu, kukanusha taarifa hiyo.

   Kwa mujibu wa Mwambene, katika gazeti hilo toleo na 0091 la Aprili 17-23, mwaka huu lenye kichwa cha habari ‘Hati za Muungano utata’, taarifa husika inakebehi hati hiyo na kujenga taswira kwamba ni ya kughushi na batili.
Linadai waandishi wawili ndiyo waliona kati ya waandishi zaidi ya 20 waliokuwepo kwenye mkutano wa Katibu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

    "Taarifa ya gazeti la Mawio ni ya kimawazo na imeandikwa pasipo shaka kutimiza malengo na maslahi binafsi wanayojua,” alisema. 

Alisema pamoja na maelezo ya Katibu Kiongozi, Sefue, gazeti hilo liliamua kwa utashi wake kukejeli na kuuaminisha umma wa Watanzana kwamba Hati ya Muungano ina utata.

        Ndipo mkurugenzi wa Gazeti hilo katika toleo lake la 0092 la Aprili 24_hadi Aprili 30 katika moja ya habari yake alisema wao hawajapata taarifa juu hayo madai ya Mwambene.

No comments: