Tuesday, April 1, 2014

YALIYOJIRI DAR ES SALAAM LEO---TCU WAJA NA MFUMO WA KUDHIBITI ADA VYUO VIKUU, PROF MGASA ASEMA HUO NDIO MUAROBAINI WAO

Kaimu katibu mtendaji wa tume ya vyuo vikuu hapa nchini (TCU) Profesa Magishi Nkwabi Mgasa akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari juu ya mfumo wa kutathimini Bei za Ada katika vyuo vikuu hapa nchini,Katika mfumo huo mpya wa kutathimini utozaji wa ada kwa mwanafunzi, Tume imezindua mfumo ambao vyo vyote vinapaswa uufuate kabla ya kumtoza ada mwanafunzi.
STORY NA KAROL VICENY---PICHA NA FULLHABARI BLOG
TUME Ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imepata muarubaini wa kudhibiti ongezeko la ada nchini kutokana na vyuo  vikuu nchini kuongeza ada kiholela bila mipangilio.

Hayo,yalisemwa mda huu na Kaimu katibu mtendaji wa Tume hiyo,profesa Mwagishi Mgasa wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari makao makuu ya Tume hiyo Jijini Dar es Salaam,ambapo alieleza wamefikia maamuzi hayo kutoka na kuwepo malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya ongezeko la karo linalotozwa na baadhi vyuo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini juu ya Mfumo huo mpya wa kutathimini vigezo vya kumtotoza mtoto ada kwa wanafunzi watakaojiunga na vyuo vikuu hapa nchini, Profesa Mgasa amesema mfumo huo umekuja katika wakati muafaka na wanaamini kuwa utapunguza kwa kiasi kikubwa adha zilizokuwa zinatokea katika vyuo vikuu ya kupanda ada kiholela
“Tumezindua mfumo wa kutathimini ada za vyuo ambao ulizinduliwa na Waziri wa elimu Dr Shukuru Kawambwa kwa lengo la kupambana onezeko kubwa la ada linalotozwa na baadhi ya vyuo vikuu hapa nchini na kwa sasa wananchi wanaangaika sana hususani wanafunzi kutokana na ada kubwa zinazotozwa”alisema Profesa Mgasa
 Vilevile Profesa Mgasa alisema mfumo huu utasaidia kupunguza ongezeko la ada nchini,na alizidi kusema kuongeza walianza kufanyia utafidi na kubaini vyou vinaweza vikajiendesha pasipo kutegemea karo kutoka kwa wananfunzi.

“Mfumu huu ni mzuri utasaidia wananchi sana,kwanza hawezekani leo vyuo vitegemee ada kwa wanafunzi kujiendesha kwani lazima chuo kitegemee asilimia75 kutoka kwa wananfunzi na asilimi 25 kutoka vyanzo vengine ili kuaacha utegemezi wa kujiendesha  kutoka kwa wanafunzi kwani itasadia kupunguza mzigo kwa wanafunzi”alizidi kuongeza profesa Mgasa

Aidha Profesa  mgasa aliwataka wanafunzi nchini kutoka vyuo vikuu mbalimbali  nchini kutolipa ada kwa kutumia Fedha za kigeni yaani Dola na kama kipo chuo kinafanya hivyo basi watoe taharifa kwenye Tume hiyo ili hatua zichukuliwe kwenye vyuo hivo.

Kuhusu wanafunzi kununua Andiko yaani( Desertation)

Profesa Mgasa alisema kwa sasa Tume hiyo imeanzisha utaratibu wa kupambana ununuaji wa Desertation na wanafunzi wa Vyuo vikuu nchini wakati wa kumaliza elimu yao.

“Kwasasa tume hii imejipanga kupambana na tabia hizi na kutoka kwa wanafunzi wanaofanya Tabia ya kununua,kwa sasa tumevitaka vyuo  vikuu na vyuo vya kati walete nakala zote za Andiko yaani  (Desertation)  ya kila mwananfunzi hapa TCU ili kubaini kama yuko mwanafunzi ambae atafanya hivyo  na kama yuko atafutiwa shahada yake”alisema Mgasa

Vilevile tume hiyo iko mbioni kuanzisha mtambo ambao utaweza kubaini watu watakanakili Dersatation za wengine.

“Kwa sasa nakipongeza Chuo kikuu Huria nchini kuanzisha  mtambo ambao unaweza kubaini wanafunzi wanaonakili Andiko yaani(Dersatation)na sisi  tuko mbioni kuweka mtambo kama huo iliuweze kupambana na watu wenye tabia hii”alisema Mgasa

No comments: