CHAMA cha Mapinduzi
CCM,kimeingia kwenye Kasfa Kubwa kutokana na Chama hicho kufanya Utapeli wa
ahadi ambao umemkumba Katibu Mwenezi Itikadi wa Chama Cha (CCM) Nape Moses Nnauye baada ya kutoa ahadi
kwa mshiriki wa shindano la Maisha Plus Bernick Mathias Kimiro wa mwaka 2012.
Utapeli, huo umethibitika jana siku
ya jumapili katika sherehe za kumtangaza mshindi wa Maisha Plus/Mama Shujaa
mwaka 2014, ambapo aliekuwa MC wa shughuli hiyo Masoud Kipanya
alipomuomba Bernick Kimiro ambae ni mshindi aliepita ainuke kutoa neno kabala
ya kukabidhi taji kwa mshindi mpya.
Aidha, baada ya kutoa shukrani zake na kumpongeza mshindi wa mwaka 2014
ambae ni Boniphace Meng'anyi Nyakena kutoka Dar es salaam, Kimiro alisema “
Naomba nitoe ya moyoni, Mheshimiwa nape alikuja kijijini akaahidi kwamba
kwaniaba ya chama cha mapinduzi kuwa watatoa nusu ya zawadi kwa kijana atakaye
kuwa mshindi wa maisha plus kwa mwaka 2012”
“na mimi ndiye niliyekuwa mshindi
kwa mwaka huo baada ya maisha plus kukamilika hakunipa zawadi zangu, wao wakajaribu
kunisaidia kumfatilia Nape wakaona anawasumbua wakaamua kulirudisha hilo swala
kwangu” alisitiza Kimaro.
Aidha Kimaro aliasema hayo akiwa
anarekodiwa na kurushwa moja kwa moja na televiheni ya Taifa TBC1, kutoka
katika kijiji cha REKEBISHA kulikofanikia shughuli hizo, za kuwapata washindi
hao ambao ni vijana na kina mama kwa upande wa mama Shujaa.
Mshindi huyo alipata zawadi ya
shilingi milioni 20, kutoka kwa Maisha Plus ambapo kwa mujibu wa Nape
alipotangaza atatoa nusu ya gharama takazo pewa mshindi kwa niaba ya chama
hivyo ni sawa na ahadi ya shilingi milioni 10 taslim ambayo ndio nusu ya
gharama zilizo tolewa na waendeshaji wa mashindano hayo.
Akiongea kwa masikitiko Kimaro alieleza
“nilienda mwenyewe ofisi za chama wakanipa namba ya Nape nikampigia nikajieleza
akaniambia nisubiri atanipigia lakini hakufanya hivyo, nikaendelea kumtafuta
kwa ujumbe mfupi wa simu (SMS) pamoja na kupiga simu lakini sikufanikiwa
kumpata wala kuongea Naye tena na mwisho namba ikawa haipatikani.
Baadae nikaamua kumfatilia ofisini
kwake lakini nikawa napewa majibu kuwa nisubiri hayupo ijapokuwa nilikua
naonyeshwa gari lake kwamba yupo ndani nikaambiwa nifate itifaki (protocol) kwa
kuandika barua nikafanya hivyo kama mara tatu bila mafanikio.
nikaomba msaada kwa Kada mmoja wa
chama akanipeleka kwa mheshimiwa Kingunge Kumbaremwiru nikamweleza suala
langu akaniambia hamna shida kwasababu ahadi ilitolewa kwa niaba ya chama
nitapewa akawasiliana na Katibu wa Chama Abdurahmani Kinana likini pia hapakuwa
na mafanikio.
Nikapelekwa kwa mbunge Wangu wa
kinondoni Iddi Azan nae akaniahidi atafatilia lakini mwisho wa siku nikaachwa njia
panda kwani sikupata msaada wowote mpaka sasa na kama unavyojua ahadi ni deni
nakiomba chama cha mapinduzi wanipatie hiyo fedha kwani waliahidi wenyewe mbona
Nyarando alitimiza ahadi zake sasa kwa Nape inakuaje?????? Alisistiza
Kimaro.
Aidha suala hilo liliwaacha midomo
wazi na kufanya wageni waalikwa wengine kushindwa kutoa ahadi zao walipopanda
jukwaani, na kuishia kuwaita viongozi wa Maisha Plus/Mama Shujaa waende ofisini
kwao ili wakaongee jinsi ya kushirikiana nao.
Kati ya waliotoa mialiko wa aina
hiyo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Yamungu
Kuyandabila ambae alikuwa ni mgeni rasmi wa sherehe hizo.
Aidha kwa upanda wa baadhi ya wageni
waalikwa walisikitishwa sana na kitendo hicho cha kiongozi wa chama tawala
kushindwa kutekeleza ahadi alizoahidi kwa kijana huyo huku wakidai kuwa wao wanamipango
mizuri kwa maendeleo ya vijana.
Akizungumza kwa masikitiko, mgeni
moja ambae alijitambulisha kuwa yeye ni kiongozi wa vijana wa chama hicho
ambae hakutaka kutajwa jina alisema” Nimepokea habari hizi kwa huzuni
kubwa na inaonesha ni jinsi gani chama changu kinashindwa kutekeleza sera zake
kwa jamii, kama chama kimeshindwa ahadi ya milioni 10 itawezekana ahadi ya
kuliondoa taifa katika janga la umaskini? Alijiuliza mchangiaji.
Pamoja, na hayo mshindi mwingine
ambae alijichukulia fedha taslimu shilingi milioni 25 kutoka Oxfan ni Mama
Shujaa Bahati Muriga mwalimu mkuu shule ya msingi Muhozya Mwanza ambae pia ni
mjasiria mali anaefanya kilimo cha chakula.
Mwandishi wa Mtandao huu ulimtafuta
Katibu Mwenezi Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Nape Moses Nnaueye kutaka
kujua Hatma ya Mshiriki huyo,pamoja na Ahadi hiyo,ambapo Nape alikana kuwa
mgeni Rasmi kwenye Michuano hiyo.
“Sikiliza Mwandishi,Sijawai kwenda
kwenye Mashindano hayo ya Maisha Plus,na Sijawai kumwahidi mtu na Kutotimiza Ni
Ahadi vizuri mkamtafuta Muandaaji wa Mashindani Masoud kipanya”
“Na hilo nasikia kutoka kwenu na
nimeona kwenye Mitandao ya kijamii,kwamba nimewai kutoa ahadi yeyote, kiukweli
sijatoa ahadi yeyote na vilevile kushiriki au kuwa Mgeni Rasmi,na hizo Ni
Habari za kutungwa na kunichafua mimi”alisema Nape.
Nape,ambaye anatoka kwenye Chama
Kikongwe Afrika ambacho kipo Madarakani,alizidi kusema chama hicho hakina
mpango wa kutoa ahadi za uongo na Kumtaka Mwandishi wa Mtandao huu amtafute
Mwandaaji ya Mashindano Masoud Kipanya amuulize kama Nape aliwai kuwa
Mgeni Rasmi.
Mwandishi wa Mtandao huu alimtafuta
Mwaandaaji wa Mashindano ya Maisha Pluss hayo, Masoud Kipanya kutaka
kujua ukweli wa Ushiriki wa Nape kuwa mgeni Rasmi katika Mashindao hayo,
Masoud,alikiri kwa Nape kutoa Ahadi
hiyo Miaka miwili iliyopita na Kushangaa kiongozi kubadilika kiasi hicho.
“Mimi nimefanya hivi makusudi
kumtangaza kwenye Runinga ili Nchi nzima ione ubabaishaji wa Viongozi wetu katika
ahadi.yeye alikuja Miaka miwili iliyopita na nyie mlikuwa Mashaidi Jinsi
alivyokuwa anatoa Ahadi nashangaa leo anavyobadilika”alisema Masoud.
No comments:
Post a Comment