.

BIBI ALIYENASWA NA MADAWA YA KULEVYA AANGUA KILIO MAHAKAMANI

BIBI wa Kinigeria, Olabisi Ibidun Cole (65), leo ameangua kilio katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar ers Salaam wakati akipelekwa kizimbani kwa ajili ya kusomewa kesi yake ya kunaswa na madawa ya kulevya yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 37.
Hakimu aliyepelekewa kesi hiyo, Frank Mushi, aliiahirisha kesi hiyo mpaka kesho ili bibi huyo ambaye hajui Kiswahili wala Kiingereza atafute mkalimani.
Cole alisema lugha anayoweza kuitumia kiufasaha ni Kiyoruba ambacho hutumiwa nchini Nigeria. Katika hali iliyoonesha kukata tamaa, bibi huyo alianza kuangua kilio akiomba Mungu amsaidie.

 
Bibi wa Kinigeria, Olabisi Ibidun Cole akipelekwa mahakamani.


About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.