Na Karoli VInsent
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam,lamlilia Aliyekuwa Mwandishi na mpiga Picha wa Kituo cha Runinga cha
Mlimani Mzee Maxmiliani,ambaye aliyefariki Gafla kwa Presha.
Kilio hicho, kimetolewa leo Jijini Dar
es Salaam na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman
Kova,wakati wa Mkutano na Waandishi Habari, Ambapo alisema wao kama Jeshi la
Polisi wamesikitishwa na Kifo cha Mwandishi wa huyo Mkongwe wa Habari na Mpiga
picha Nchini.
“Sisi Jeshi la polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam,Tumesikitishwa sana na Kifo cha Mzee wetu huyo Bwana
Maxmiliani,kwani amekuwa akitoa Mchango mkubwa,kwetu Jeshi la
Polisi hususani Kanda hii ya Dar es Salaam kwa kuhakikisha Taarifa
zinafika kwa Wananchi kutoka kwetu kwa wakati Muhafaka,”
“Kwani Jeshi la polisi
limekuwa likifanya Kazi kwa ukaribu mkubwa na Wanahabari kwasababu wamekuwa
wakitoa Mchango mkubwa katika kuhakikisha Tarifa zetu kwa Umma”Alisema Kova
Kamishna, Kova alizidi
kusema kutokana na Kugushwa na Msiba huo ameamua Kutoa Pesa ya Rambirambi
shiringi Laki Moja,
“ Kutokana na Kugushwa
na msiba huu mimi Binafsi nimetoa Fedha Taslim shiringi Laki moja,natunajaribu
kujadiliana na Kanda Maalum tujue tutafanya Utaratibu Mwingine”Alizidi
kusema Kova
Kwa upande wake
Waandishi Mbalimbali waliozungumza na Mwandishi wa Mtandao huu hawakusita
kuonyesha kusikitishwa na Msiba huo,kati yao ni Mwandishi Mwandamizi wa
habari kutoka kituo Cha Runinga cha Chanel Ten Mzee Kibwana Dachi.
Ambapo,alisema
amesikitishwa sana Kifo cha Mwandishi huyo wa Mlimani Tv,kwani yeye amemjua
Miaka mingi sana, kutokana akitoa mchango mkubwa katika Taaruma hii ya Habari
“Kwanza ngoja niseme,
mimi nimeanza kumjua mzee maxmiliani siku nyingi sana,kusema kweli tasnii hii
ya Habari imepoteza mtu muhimu sana kutokana kwa kufanya kazi kwa umakini sana
na vilevile kushirikiana na wenzake bila ugomvi wowote”alisema Kibwana Dachi.
Kibwana Dachi,ambae ni
Mchambuzi wa Masuala Mbalimbali ndani Nchi na nje,aliwataka vijana
wanaochipukia katika taaruma hii,kuiga mfano wa Mzee Maxmilian ili waweze
kupata Mafanikio.
Naye,Msomi wa Masuala
ya Habari kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na vilevile ni Mwandishi Gazeti
la Tanzania Daima,mwandishi John Magigi.alisema Taaluma ya Habari Nchini
Imepoteza mtua Makini na mwenye Moyo wa Kujituma.
No comments:
Post a Comment