Friday, May 30, 2014

BREAKING NEWZZ : GEORGE TYSON AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI MBAYA YA GARI MKOANI MOROGORO--TZAMA PICHA ZA GARI LAO NA PICHA ZAO KABLA YA AJALI--R.I.P TYSON

George Tyson

George Tyson
Muongozaji mkongwe wa filamu nchini Tanzania  mwenye asili ya Kenya, George Tyson amefariki Dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari   wakati wakitokea kwenye hafla ya kuadhimisha miaka miwili ya kipindi cha luninga cha The Mboni Show mkoani Dodoma kufuatia gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Noah kupasuka matairi   na kuangukaeneo la Gairo mkoani Morogoro majira ya saa moja jioni.
Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha na wengine kupata majiraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika  hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza safari ya kurudi Dar es Salaam
Awali Tyson aliwahi kuwa mume wa muigizaji nyota wa kike wa Bongo Movie, Yvonne Cherry ‘Monalisa’ aliyeza nae mtoto mmoja wa kike anayeitwa Sonia.
Atakumbukwa kwa ucheshi, ukarimu na busara zake, Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali pema peponi Ameen.

Gari alilopata nalo ajali Director George Tyson na picha za saa 4 kabla ya tukio

Dj Choka ambae kwa sehemu kubwa alikua kwenye safari moja ya Dodoma na Marehemu George Tyson, ameandika kwenye
Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.30 AM
Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.12 AM
Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.38 AM
Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.50 AM
Kwenye hii safari, George Tyson aliambatana na mtangazaji Mboni Masimba wa The Mboni show.
Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.58 AM


No comments: