Friday, May 30, 2014

KAMA ULISKIA ILE STORY YA KATIBU MKUU WA CCM KINANA KUGOMBEA URAIS MWAKANI--UNDANI WAKE HUU HAPA

Na Karoli Vinsent

       KATIBU wa chama cha Mapinduzi CCM,Abdulrahman Kinana,anatarajiwa Kugombea Urais kwenye Uchaguzi mkuu mwakani  2015.

Taarifa hizo ambazo Mtandao huu umedokezwa,zinasema  kitendo cha Katibu mkuu huyo kuingia kwenye Kinyanganyiro hicho zinalenga Kuwanyamazisha Makada mbalimbali ndani ya Chama hicho ambao wamekuwa wakitumia kila Njia kuhakikisha wanashika nafasi hiyo ya Urais kwenye uchaguzi mkuu mwakani.


       Makada mbalimbali ndani ya chama cha Mapinduzi CCM ambao wamekuwa wamejitokeza Hadharani kutaka nafaisi hiyo ni , Edward Lowassa,  Bernard Membe,Stivin Wassira, Frederick Sumaye,William Ngereja,January Makamba,Samweli Sitta mala kadhaa wamekuwa wakiitaji Nafasi hiyo.

      Chanzo hicho kinasema sababu kuu inayomfanya katibu mkuu huyo Wa CCM,kuingia katika Kinyanganyilo hicho ni kutokana na Uwezo aliouonyesha ndani ya Chama na  kuanza kukubalika kwa Wananchi.

   Akilizungumizia hili Mjumbe wa Halmashauri kuu NEC ya Chama cha Mapinduzi CCM,ambaye anatokea  Mikoa ya Kusini,huku hakutaka Jina lake litajwe Kwenye Mtandao huu anasema,kasi ya Kinana inatishia wasaka Urais.

        “Sikufichi Mwandishi kasi aliyoanza nayo katibu wetu Kinana ni kubwa sana,Maana chama kilipoteza mvuto kwa Wananchi ila baada ya kuchagulwa Jembe hili Kinana,hari imekuja kwenye chama chetu na Sikufichi huyu lazima awashangaze wengi mwakani kwani anakila aina ya Sifa ya kugombania Urais”

    “Na lazima wasaka Urais, ambao wanapita kwenye makanisa na misikitini wakiomba Huruma ya wananchi ili waonekane wasafi,wapate madalaka kiukweli huyo mzee Kinana lazima agombanie Urais”alisema Mjumbe huyo wa Halamshauri Kuu ya NEC.

     Duru zinasema Katibu mkuu huyo,kuanza kuonyesha Dalili hizo kunazifanya zile Kambi za Wasaka Urais wa Chama hicho,kuanza kuweweseka na kushindwa wajue wafanyaje ili waweze kuipunguza nguvu kasi ya Kinana.

      Mbio hizo za Kinana zinameibuka ikiwa ni Miezi michache kupita baada ya Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi (CCM),kuwafungia wasaka hao wa Urais kwa mda wa Miezi 12,kutafanya Vitendo hivyo vya kutaka Urais.

       Makada hao ambao, waliohojiwa niWaziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond,  ambaye pia ni Mbunge wa Monduli,Edward Lowassa,  wengine waliohojiwa kwa nyakati tofauti katika ukumbi maarufu kama White House mjini Dodoma ni Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye pamoja na aliyepata kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.

       Viongozi hao walihojiwa kutokana na kile kinachoaminika ni kuanza kampeni za kusaka urais 2015 kupitia CCM kabla ya wakati rasmi kuwadia, huku wakichezeana rafu na matumizi makubwa ya fedha yakihusishwa.

Akizungumzia kitendo hicho cha Katibu mkuu huyo wa Chama kikongwe kabisa Afrika ambacho kipo Madarakani ,Msomi wa Masuala ya kisiasa kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Seiph Yahaya,alisema kitendo hicho cha Katibu Kinana kuingia kwenye Kinyang”anyilo alisema kinaweza kukipeleka chama hicho kwenye misuguano isiyokuwa na Lazima kwani uwezo wake hawezi kuendana na Kasi za Siasa

    “Kiukweli ndugu mwandishi acha Nikwambie, ukweli uwezo wa Kinana haendani na kasi ya sasa ya Taifa lilipofikia kwani Taifa linamabadiliko mengi sana hebu angalia changamoto atakzoachiwa na Rais Kikwete Kinana haziwezi”

       “Na kama chama kupitia Halmashauri kuu yaani NEC wakiamua kumpitisha Kinana wajue chama ndio kinachafuka na kuingia kwenye matatizo,kwani makada wasaka Urais watatengeneza bifu kubwa kwa Kinana”alisema Seiph Yahaya msomi wa Masuala ya Siasa kutoka chuo Kikuu cha Dodoma.

       Kwa mujibu wa Kada wa chama cha Mapinduzi Kutoka katika Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM.ambaye naye akutaka kutajwa kwenye Mtandao huu alisema Nguvu kubwa ya Kinana imetokana na msukumu mkubwa kutoka kwa Waziri Mkuu wa sasa mizengo Pinda ambaye amekuwa akimbeza,Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward lowassa kwamba hana sifa ya kuwa rais.



No comments: