Mgeni rasimi katika uzinduzi
wa tawi la wanafunzi vyuo vikuu wanachama wa chama cha Kiswahili
Afrika Mashariki (CHAWAKAMA)afisa utamaduni mkoa wa Iringa Kenneth
Komba wa tano waliosimama kutoka kushoto akiwa na wanachama wa chama
hicho tawi la chuo kikuu cha Iringa mara baada ya kuzindua tawi hilo
………………………………………………………………………..
Na Mwandishiwetu blog WANAFUNZI wa chuo kikuu cha Iringa zamani Tumaini
wamewataka wajumbe wa bunge la katiba kuhakikisha wanapigania
lugha ya Kiswahili ili iweze kupewa nafasi kubwa katika katiba mpya.
Rai
hiyo imetolewa na mlezi wa wanafunzi wa chama cha Kiswahili
Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) Tullah Tweve wakati wa uzinduzi wa
tawi hilo chuoni hapo jana
Tweve alisema kuwa hakuna faida kubwa kwa taifa kama
kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha kuu katika taifa na hata
kuitumia katika kufundishia mashuleni na vyuo.
Alisema wakati huu ni wakati mzuri wa Taifa kuweza
kurekebisha makosa yaliyokuwepo katika kuchanganya lugha na kukumbatia
lugha za mataifa mengine na kuacha lugha yetu .
Hata hivyo alisema kuwa yeye kama mwalimu wa Kiswahili
katika chuo hicho moja kati ya mambo ambayo anayapa kipaumbele ni
pamoja na kiswahili kupewa kipaumbele.
Kwa upande wao wanafunzi wanachama wa Chawakama
walisema kuwa walengwa wakuu wa chama hicho ni wanafunzi wa vyuo
vikuu wanaosoma Kiswahili na kuwa wanachama ni nchi tano barani
Afrika kama Tanzania ,Uganda , Kenya ,Rwanda na Burundi lea kusihiriki
makondamano mbali mbali barani Afrika .
Pia walisema kuwa msukumo wa kuanzisha Tawi hilo ulitokana
na jitihada za mwalimu Tulla Tweve na Albart Chalamila na kuwa tawi
kwa sasa linawachama zaidi ya 60.
Walisema kuwa chama hicho kimeanzishwa mwaka 2002 na
kuwa katika chuo cha Iringa tawi hilo lilianzishwa mwaka 2010 na
kuwa mbali ya kutokuwepo kwa tawi ila bado wanafunzi wa somo la
kiswahili waliende
Aidha walisema changamoto kubwa ni kukosekana kwa fedha
za kuendeshea chama pamoja na chama hicho kutotambulika kwa kuwa na
uongozi wa unaojulikana na chuo hicho.
Afisa utamaduni mkoa wa Iringa Keneth Komba mbali ya
kuwashukuru wanachama wa chama hicho cha Chawakama kwa kuenzi
kiswahili bado alisema kuwa jitihada hizo kubwa zilizoanzishwa na
chuo hicho.
Hata hivyo alisema kuwa wenye uwezo wa kukuza
kiswahili ama kubomoa lugha ya kiswahili ni wasomi wenyewe ambao
wamepelekea kuyumbisha lugha .
Komba alisema kuwa mikataba mibovu ya kifisadi katika Taifa inasababishwa na lugha ya kiingereza ambayo wengi wa “Tunatambua kuwa duniani kuna lugha zaidi ya 16 ikiwemo
lugha ya kiingereza ,kifaransa kirusi na kiarabu na lugha mbali mbali
huku katika afrika lugha kuu ni kiswahili ambao lugha hiyo imekuwa
ikiendelea kukua zaidi barani afrika “
|
No comments:
Post a Comment