SIKU chache Kupita Baada,Kampuni ya
kufua umeme kwa njia ya Gesi,Songas limited kutishia kuzima mitambo
yake,kutokana na ilichokiita.shirika la umeme Nchini(TANESCO) kushindwa kulipa
deni linaofikia Dola za Kimarekani 72.8 milioni(karibu sh 116.4 bilioni za
kitanzania).
Naye,Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la
Umeme Nchini(TANESCO) Eng Felchesmi J Mramba,ameibuka na kusema Songas
wamevunja makubaliano kwa kitendo chake ,cha kutumia vyombo vya Habari kudai
deni hilo.
Maneno ya Mkurugenzi huyo ameyatoa Leo
Jijini Dar Es Salaam wakati alipokuwa anafanyiwa Mahojiano na Mwandishi wa
Mtandao huu juu ya Taarifa zilizoripotiwa na Gazeti moja linalotoka kila wiki
juu ya Madai ya Madai hayo,ambayo yatapelekea Nchi kuingia Gizani.
“Mahusiano ya Songas na Tanesco ni
ya kibiashara,na utaratibu kudai deni uko wazi.sasa nashangaa kampuni ya Songas
wanatumia kudai kupitia Gazeti la Mawio,kiukweli hajafanya busara,”
“Hivi na mimi pia wanataka nitumie
Vyombo vya Habari kujibu hayo madai wanayoyasema?mimi nawaomba Songas watumie
utaratibu mzur
i wa kudai hayo madai lakini sio huo wanaoutumia sasa”alisema
Mramba.
Vilevile Kuhusu vitisho wanavyotoa
Kampuni hiyo ya Songas Juu ya Kuzima mitambo yao endapo shirika hilo
litakaposhindwa kulipa Deni hilo,Eng mramba alisema kwa sasa hawezi
kulizungumzia hicho kitisho wanachokitoa na hatatoa utaratibu wote kwa wananchi
na vilevile akawaomba wananchi wasiwe na wasiwasi Juu ya Taarifa hizo
Taarifa za Songas Kuzimia mitambo yao ziliripotiwa na Gazeti moja la
Wiki ambalo katika toleo hilo lilisema,Shirika hilo la Umeme limepuuzia amri ya
Waziri wa Nishati na Madini,profesa Sospeter Muhongo ambayo iliwataka shirika
hilo kuilipa Kampuni ya Songas Deni lake haraka sana,
Lakini kwa kupitia Barua ya Mkurugenzi
mtendaji wa Songa,Christopher Ford aliyoiandikia shirika la Tanesco ilisema
mpaka mda huu Tanesco walishindwa kulipa deni hilo.
Barua hiyo ilizidi kusema madeni
yanaivuruga uwezo wake wa Kiutendaji,hata hivyo,Ford anasema Songas inataka
Kulipwa mara kwa mara Dola 30 milioni kutoka kiasi inachokidai Tanesco ili
kukidhi mahitaji yake.
Kampuni hiyo inalalamika kuwa
haijapokea malipo yeyote kwa mfumo wa malimbikizo kama Tanesco
walivyohaidi mbele ya Waziri wa nisharti na Madini .
No comments:
Post a Comment