Friday, May 2, 2014

MIGOGORO NDANI YA WIZARA YA MALI ASILI NA UTALII MCHUNGAJI MSIGWA AIBUKA,SOMA ALICHOZUNGUMZA NA MTANDAO HUU



    Na Karoli Vinsent

         SIKU moja kupita Baada ya Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete kupuuza maoni ya Kamati ya bunge ya Ardhi,Maliasili na mazingira ,kwa kitendo chake cha kumrudisha ofisini, Mkurugenzi wa Wanyama Pori,Profesa Alexander Songorwa,

       Ambaye, aliyetimuliwa kazi na Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu miezi miwili iliyopita,kwa madai ya kushindwa kutekeleza Majukumu yake ipasavyo,


        Vilevile, Nyalandu alifuata maoni na mapendekezo ya Kamati ya bunge ya Ardhi,Maliasili na mazingira,ilipotoa Taarifa Bungeni juu wakati ikisitishwa kwa oparesheni tokomeza ujangili,ambapo ripoti hiyo ilimtuhumu  waziwazi Mkurugenzi wa Wanyama Pori,Profesa Alexander Songorwa,kwa kushindwa kusiamia majukumu yake na kupelekea matatizo kwa wananchi.

        Hivi leo naye Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mchungaji Peter Msigwa amemvaa,Waziri  Nyalandu na kusema ndio kinara cha matatizo kwenye wizara hiyo kutokana na kuwaweka watu wasiokuwa na sifa na uwezo, akiwemo Mkurugenzi wa Wanyama pori Paul Sarakilya.

       Kauli hiyo ya Msigwa ameitoa leo wakati alipokuwa afanyiwa mahojiana na Mwandishi wa Mtandao huu,juu ya hali ya sintofamu ndani ya Wizara hiyo Juu ya kitendo cha waziri wa wizara hiyo kwa kushindwa kuweka Nidhamu kwa wafanyakazi.

      “Leo namshangaa sana Waziri,kwa mfano  waziri Nyalandu alimuondoa Mkurugenzi wa Wanyama pori Profesa Songorwa na  akamrudiswa kwenye nafasi hiyo Paul Sarakilya ambae anarekodi chafu,wakati wa kipindi chake amekuwa na rekodi chafu katika kipindi chake Tanzania ikapanda na kuwa kinara kwa vitendo vya Ujangili na kupelekea Tanzania kuingia Sifa mbaya”

         “Harafu tumeshuhudia katika kipindi Cha tokomeza Ujangili huyu  Sarakilya amepelekea madhara makubwa sana watu kufa pamoja kukiukwa haki za Binadamu,leo waziri anamrudisha mtu huyu hata mimi kwenye hutuba yangu kwenye Bunge la bajeti nitalizungumzia hili, maana kunakitu waziri anataka kukifanya hapa”alisema Msigwa

       Msigwa ambaye ni Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendereo Chadema,alizidi kusema kitendo cha kumfukuza mkurugenzi huyo wa Wanyamapori Profesa Songorwa alivunja Kanuni.

      “Mimi nashangaa leo Waziri anamwachisha kazi mtu kwa kutumia (Press Conference),maana kunataratibu za kumfukuza kazi,lakini Waziri hana uwezo wa kufukuza mtu kazi,anatakiwa kutoa mapendekezo kushauriana na katibu mkuu wa Wizara  na kupeleka mapendekezo kwa katibu kiongozi ndio mwenye jukumu la kumfukuza kazi,maana watendaji wote wale wa wizara wako chini ya katibu mkuu kiongozi,na hili linatupa wasiwasi sana kuhusu waziri na Wizara hii”alizidi kusema Msigwa

        Katika hatua nyingine msigwa alimtaka Rais Kikwete aingilie kati mgogoro ulioko ndani ya maliasili,lasivyo  akipuuzia,itapunguza uwajibikaji ndani ya Wizara Hiyo.  

No comments: