Kituo cha sheria na haki za binadamu kupitia kamati
yake maalum ya katiba SCOC imeitaka
mamlaka ya juu ya nchi kuupa kipaumbele
mgogoro ambao umetokea kwenye bunge maalum la katiba ili kunusuru mchakato wa
kupata katiba mpya.
Hayo yamesemwa
leo jijini dar es salaam na mwenyekiti wa kamati hiyo ya katiba dkt KHOTI KAMANGA
wakati akizungumza na wanahabari ambapo amesema kuwa kamati yake imesikitishwa
sana na mwenyendo mbovu wa bunge maalum la katiba na hatimaye kuparanganyika kwa
chombo hicho muhimu kilichokuwa na kazi ya kujadili na kuboresha rasimu ya
katiba kama ilivyowakilishwa na tume ya mzee warioba.
Dkt KAMANGA amesema kuwa ili kuurudisha mchakato wa
katiba katika mstaari ni lazima viongozi wa juu ya nchi huku akimtaja rais
KIKWETE kuuchukulia mgogoro huo ambao umeligawa bunge maalum katika hali ya
ukubwa na kutafuta mbinu za kuwapatanisha ili wale waliotoka bungeni kurejea na
kutafuta katiba mpya kwa pamoja.
Aidha amesema kuwa ni lazima wabunge na watanzania wote
kujenga utamaduni wa kusikilizana na kushauriana na kupokea ushauri ukiwemo ule
unaotokana na wataalam na wazalendo bila kupuuzia mawazo yao kwani yapo
yanayotaka kuunusuru mchakato huo,
Aidha katika hatua nyingine kamati hiyo imeshauri
kwamba katika mchakato wa kupata katiba mpya ni lazima bunge lizingatie maoni
ya wananchi yaliyopo ndani ya rasimu ya katiba na iwe ndio agenda kuu tofauti
na sasa ambapo misimamo ya vyama ndio imeonekana kujadiliwa sana kuliko rasimu
yenyewe.
Wanahabari mbalimbali wakisikilza |
No comments:
Post a Comment