Tuesday, May 13, 2014

UNDP SASA YAAMUA KUSAIDIA VITA DHIDI YA UJANGILI


  Kiongozi wa UNDP  na waziri mkuu wa zamani wa new Zealand ,HELEN CLACK leo ametoa wito kwa serikali na duniani kote kuongeza mapambano dhidi ya ujangili wa tembo na biashara haramu katika bidhaa za wanyamapori  kama vile pembe za ndovu.
        
    Akizungumza na wanahabari leo jijini dar es salaam amesema kuwa uhalifu kama vile ujangili na biashara ya pembe za ndovu una madhara makubwa kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu katika nchi zinazoendelea kwa kupora mali,kuharibu maliasili kwa vizazi vijavyo,kuchochea uhalifu na rushwa na kudhoofisha jamii na usalama wa taifa,uhalifu huu unaweka wanawake ,watoto na watu wengine katika umaskini,kwenye matatizo zaidi na hatari kubwa “amesema”.
          Wakati Tanzania ikiwa ni mashuhuri kwa wingi pamoja na aina ya rasilimali ya wanyamapori hasa tembo,ni dhahiri kuwa ujangili wa tembo na biashara haramu ya pembe za ndovu Tanzania na barani Africa imeongezeka kwa kasi kubwa katika miaka ya hivi karibuni na hivyo kuwa tishio kwa maisha ya tembo na vifaru.
        
           Kiongozi huyo amesema kuwa kuna haja ya utekelezaji wa nguvu ya sheria kupunguza mahitaji ya bidhaa haramu ya pembe za ndovu zinazouzwa kinyume na sheria, aidha  mtawala uyo ameahidi kuwa shirika lake la umoja wa mataifa lina nia ya kuunga mkono mapambano dhidi ya ujangili kwa kusaidia katika utawala na utawala wa sheria,kuondoa umaskini,na ulinzi wa mazingira kwa kusaidia serikali na wadau wengine.



No comments: