Hawa ndio viongozi wa panya road na mbwa mwitu ambao tayari wameshakamatwa |
Maeneo
yaliyoathirika ni Kigogo, Magomeni, Tabata, maeneo yote yanayozunguka mto
Msimbazi, maeneo ya Mbagala nk. Msako
huu unaendelea kufanywa na askari wa vikosi maalum ambao wamepewa kazi ya
kuhakikisha kuwa vikundi hivyo haviibuki tena na vinatokomezwaa kabisa kwa kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo
vya kuvamia kwa mkundi wananchi ambao hawana hatia
Kamishna kova ambaye amezungumza na wanahabari muda mfupi uliopita |
Imegundulika pia kwamba vijana hawa wanatumia dawa za kulevya aina ya bangi na wengine hujichoma sindano na kuwafanya iwe rahisi kujihusisha na matukio ya uhalifu. Vijana hao hupenda kushiriki katika ngoma kama Mnanda, Mchiriku, Kigodoro, Kanga moja nk. ambazo kwa kawaida huchezwa hadi usiku wa manane.
Wakitoka katika ngoma hizo hujikusanya pamoja na kufanya matukio ya uporaji kwa mtu wanayekutana naye, kufanya uvunjaji katika majumba na wakati mwingine wana mtindo wa kugema mafuta ya diesel au petrol katika matanki ya malori yanayosafirisha mafuta.
Operesheni kali inafanyika katika maficho ya wahalifu hao ikiwa ni pamoja na daraja la River side, Kigogo darajani, Manzese, maeneo ya Tandale pamoja na maeneo mengine ya maficho mkoa wa Kipolisi Temeke.
Tunawasiliana
na Maafisa utamaduni wa Wilaya zote za Mkoa wa D’Salaam kusimamisha utoaji wa
vibali wa ngoma za usiku ambazo hazina tija.
Pia Jeshi la Polisi linafuatilia na kuwavizia vijana wanaopora watu wanaotoka katika sherehe za usiku kama
vile Harusi na wanaotoka katika mikesha ya Ibada na sehemu zozote zenye mikusanyiko.
Aidha Jeshi la Polisi wanapambana na vijana
wanaowavizia watu katika vituo vya mabasi pindi wanapotoka alfajiri kwenda
katika shughuli zao za kila siku.
Wanahabari |
Oparesheni
hii ni endelevu na ya kudumu hadi kero hii ya vibaka itakavyokwisha kabisa.
Baadhi ya majina waliokamatwa ni kama ifuatavyo:-
1. DANIEL
PETER @ MALUNDE, miaka 25, mkazi wa Yombo Kigunga
2. MWISHEHE
ADAM, miaka 35, mkazi wa Mtoni mashine ya maji
3. MOHAMED
SAID, miaka 32, mkazi wa Mtoni
4. JAKAMA
ALPHONCE, miaka 23, mkazi wa Mtoni Kilakala
5. HAMADI
MDUDU, miaka 25, mkazi wa Mbagala
6. SALUM
MUSA, miaka 25, mkazi wa Kiwalani
7. ANTHONY
DANIEL, miaka 20, mkazi wa Mashine ya maji
8. FIDELIN
ANTHONY, miaka 18, mkazi wa Kigogo
9. HAMZA
MAZUMA, miaka 19, mkazi wa Kigogo
10.
MGANGA ABEID, miaka 20, mkazi wa Kigogo
11.
SAID ABEID, miaka 19, mkazi wa Kigogo
12.
SALUM NYENJE, miaka 36, mkazi wa Chamazi
13.
DOMINICK PETER miaka 22, Mkazi wa Kigogo
14.
KULWA ABEID, miaka 20, mkazi wa Mabibo
15.
MUSA IBTRAHIM, Miaka 20, mkazi wa
Magomeni
16.
HUSSEIN SHABAN, miaka 22, Mkazi wa
Magomeni
S.
H. KOVA
KAMISHNA
WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment