KLABU ya Manchester City imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka nchini England baada ya kufanikiwa kuwafunga West Ham mabao 2-0 katika uwanja wa nyumbani wa Etihad. Wanaume wa Manuel Pellegrini walijua wazi kuwa ushindi katika mechi hiyo utawapatia ubingwa wa pili ndani ya misimu mitatu bila kujali matokeo ya Liverpool dhidi ya Newcastle.
Samir Nasri alikuwa wa kwanza
kuifungia Man City bao la kuongoza katika dakika ya 6` tu ya mchezo huo
uliovuta hisia za mashabiki wengi wa soka duniani.
Bao la pili la Man City lilifungwa dakika ya 49` kupitia kwa nahodha wake Vicent Kompany na kuihakikishia City ubingwa wa EPL.
Liverpool walitoka nyuma kwa bao
1-0 na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle, lakini
ushindi wa Man City umewafanya washindwe kukata kiu ya kutotwaa ubingwa
kwa miaka 24, sasa imefikia 25. Tumemaliza kazi: Vincent Kompany akizingirwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao la pili
No comments:
Post a Comment