Sunday, May 11, 2014

RAMBIRAMBI MSIBA WA BALOZI WA MALAWI

tff_LOGO1
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha Balozi wa Malawi nchini, Flossie Gomile-Chidyaonga kilichotokea juzi (Mei 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Balozi Gomile-Chidyaonga ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania mwaka 2011, alikuwa Naibu Balozi wa nchi hiyo Uingereza alifikwa na mauti baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Msiba huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu nchini kwani, Balozi Gomile-Chidyaonga ndiye aliyefanikisha ujio wa timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) ambayo Mei 4 mwaka huu ilicheza mechi ya kirafiki na Taifa Stars jijini Mbeya.
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Balozi Gomile-Chidyaonga, Ubalozi wa Malawi nchini na Chama cha Mpira wa Miguu Malawi (FAM), na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments: