Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome
Sijaona (wa pili kushoto) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki
Okada, wakiongozana wakati walipokuwa wakielekea kutembelea kiwanda cha
kukamua mafuta ya Ufuta cha Takemoto kilichopo Nagoya nje kidogo ya
Jiji la Tokyo Japan, jana Mei 22, 2014, akiwa katika ziara yake ya
kikazi nchini Japan. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na ujumbe wake wakipata maelezo kuhusu kiwanda hicho kinavyofanya kazi
hadi kupatikana mafuta ya Ufuta, wakati walipofika kiwandani hapo
kujionea kutembelea na kujionea shughuli za uzalishaji, jana Mei 22,
2014. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa Kiwanda cha kukamua mafuta
ya Ufuta cha Takemoto, Akira Ogawa, jinsi mbegu za ufuta zinavyoanza
kuandaliwa kuelekea katika mashine za kukamua mafuta. Hapa ni hatua ya
kwanza zinaposhushwa mbegu hizo na kuingia moja kwa moja kwenye mitambo.
Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa wa Kiwanda cha Mafuta ya
Ufuta cha Takemoto, Akira Ogawa, jinsi mbegu za ufuta zinavyosafiri
hadi kufika katika Kinu cha kuzisaga hadi kupatikana mafuta hayo, wakati
alipotembelelea kiwanda hicho kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la
Tokyo nchini Japan, jana Mei 22, 2014. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na mkewe Mama Asha Bilal, wakionyeshwa mbegu za ufuta na Ofisa wa
Kiwanda cha kukamua mafuta ya Ufuta cha Takemoto, Akira Ogawa, wakati
alipotembelelea kiwanda hicho kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la
Tokyo nchini Japan, jana Mei 22, 2014. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment