Timu
ya Mbeya City inaondoka leo usiku (Mei 22 mwaka huu) kwenda Sudan kushiriki
michuano ya Kombe la Nile Basin inayoanza kutimua vumbi kesho (Mei 23 mwaka
huu) jijini Khartoum, Sudan.
Kikosi
cha Mbeya City chenye watu 25 wakiwemo wachezaji 20 kinaondoka saa 2.55 usiku
kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi ambapo kesho (Mei 23 mwaka huu) saa
5 asubuhi kitaunganisha ndege nyingine hadi Khartoum.
Msafara
huo wa kikosi hicho ambao utawasili Khartoum saa 7.30 mchana kwa saa za huko
unatarajia kurejea nyumbani Juni 5 mwaka huu iwapo timu hiyo itafanikiwa hatua
ya mwisho ya mashindano hayo.
Michuano
ya Nile Basin imeanzishwa mwaka huu na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu
Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), na inashirikisha timu zilizoshika nafasi za
pili katika ligi za nchi wanachama wa baraza hilo.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment