Saturday, May 24, 2014

MBWA MWITU NA PANYA ROAD WAMKASIRISHA KAMISHNA KOVA,AUNGURUMA WIKIEND HII,SASA NI JINO KWA JINO HADI KUKOMESHA WAHUNI HAO

Na Karoli Vinsent

        Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanya msako na doria katika maeneo mbalimbali ya jiji   hilo,Ili, kuthibiti makundi ya uhalifu wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na vijana wahuni wasio na kazi maalum maarufu kwa jina na MBWA MWITU au PANYA ROAD ambao wamekuwa wakipelea Uvunjifu wa Amani katika,Maeneo mbalimbali.

          Hayo,yalisemwa leo Jijini Dar es Salaam,na Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova,wakatika wa Kikao cha Dharula alichokitisha  na Makamanda mbalimbali wa Jeshi hilo Jijini Hapa chenye lengo la kupambana na Vikundi vya Hivyo vya Uharifu.


        Ambapo Jeshi hilo limewatoa Hofu wakazi wa Dar es Salaam baada yaTaarifa za Awali kwenye Vyombo vya Habari kuhusu Vikundi hivyo.

      Ambapo Kamishna Kova alisema Maeneo yote vijana hao waliopo kama vile Kigogo, Magomeni, Tabata, Manzese na maeneo ya Mbagala, wamepangwa askari wa kutosha wa doria ili kuthibiti mlipuko wowote wa vitendo vya kihuni vyenye ishara ya uhalifu vinavyoleta hofu kwa wananchi.

       Kova,Alizidi kusema vijana hao hawana uwezo tena wa kufanya uhalifu katika makundi yao kutokana na mpango kazi uliopangwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum.

       Aidha,Kova alisema kwa umakini wa Jeshi hilo katika Kupambana na Vitendo hivyo vya Uharifu, teyari Jeshi hilo teyali Limewatia Nguvuni, viongozi (Ring Leaders) sita (06) wa vikundi hivyo .

        Kamishna Kova,aliwataja Vijana hao,ambao ni ATHUMAN S/O SAID, Miaka 20, Mkazi wa Kigogo,JOSEPH S/O PONELA, Dereva Bodaboda, Mkazi wa Kigogo Mkwajuni,CLEMENT S/O PETER, Miaka 25, Fundi Selemara, Mkazi wa Kogogo,ROMAN S/O VITUS, Miaka 18, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kigogo. MWINSHEHE S/O ADAM, Miaka 37, Mkazi wa Temeke Mashine ya maji,pamoja na DANIEL S/O PETER, Miaka 25, Mkazi wa Yombo.
Katika Hatua Nyingine Jeshi Hilo la Polisi limesema   

          Pamoja na kuthibiti vitendo hivyo kutoka kwa vijana hao, umeibuka mtindo wa watu, kutuma ujumbe  mfupi  au simu za mkononi wakieleza uvumi kwamba maeneo yao yamevamiwa na makundi Mbwa Mwitu au Panya Road.


         Vilevile Jeshi hilo lilisema Mtindo huo wa uvumi umeenea sana maeneo ya Kigogo, magomeni, mansese na Tabata. Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kuhusu mtindo huo ukome kwani watu hao wanasababisha hofu kwa wananchi bila sababu na huku, Jeshi la hilo la Polisi likibainisha kuwa hakuna tukio lolote ambalo limefanyika maeneo hayo au kuripotiwa kituo chochote cha Polisi katika kipindi cha wiki hii ambapo uvumi umeenea sana.
Uchunguzi  umebaini kwamba chanzo cha uvumi huu ni kwamba tarehe 18/05/2014 na 20/05/2014 palitokea mauaji ya vibaka wawili waliohusishwa na makundi haya na kwamba kulikuwa na hofu kuwa baada ya mazishi ya vijana hao 

vijana wenzo wangeweza kulipiza kisasi ndio maana pakawa na uvumi  wa jumbe mbalimbali zilizoleta hofu.

No comments: