Rais wa jamhuri ya muungano Tanzania dk JAKAYA MRISHO KIKWETE ametakiwa kuchukua hatua kali dhidi ya kikundi cha mihadhara ya kiislam Tanzania maarufu kama UAMSHO ikiwa ni pamoja na kikifuta kikundi hicho kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kikundi hatari na hakiitakii mema nchi ya Tanzania
Hayo yamesemwa leo jijini dar es salaam
na bw HAMAD TAO ambaye ni mwenyekiti wa taasisi inayojihusisha na kujenga
undugu kati ya dini ya CHRISTIAN AND MUSLIM BROTHER HOOD SOCIETY ambapo katika mkutano na wanahabari mapema leo
taasisi hiyo imesema kuwa kikundi cha uamsho hawana lengo nzuri na nchi ya Tanzania
kuutokana na matamko yake ambayo imekuwa
ikiyatoa ya vitisho dhidi ya watu mbalimbali pamoja na dini nyingine ambapo
amesema kikundi hicho kinasababiosha uhasama baina ya dini na dini.
HAMAD TAO ambaye ni mwenyekiti wa
taasisi hiyo amesema kuwa kikindi cha uamsho hakina tofauti na vikundi vingine
vya kidaidi duniani huku akienda mbali na na kukifananisha na vikundi kama
ALCAIDA,BOCO HARAM NA ALSHABABU.
“sisi tumekuja hapa kwa upendo na
kuipenda nchi yetu tunaiomba serikali ya Tanzania isiwafungie macho hawa watu
wanaounda kikundi hiki kwani ni hatari kwa amani tuliyonayo”alisema TAO
Aidha taasisi hiyo imesema kuwa
tangu kuanzishwa kwa kikundi hicho matukio ya kigaidi Zanzibar kama kumwagiana
tindikali,makanisa kuchomwa moto na ugaidi mwingine umekuwa ukiongezeka kwa
kasi huku wakikwepa kuwahusisha uamsho moja kwa moja kuhusika na uhalifu huo,
No comments:
Post a Comment