WASANII wa Bongo Movie, muziki wa
dansi, taarab, maigizo na tamthilia wametangaza kuzunguka nchi nzima wakiwa na
kamati ya Tanzania Kwanza Nje ya Bunge Maalum la Katiba kwa lengo la kutangaza
amani kwa vijana wa rika lote bara na visiwani.
Baadhi ya wasanaii hao ni pamoja na
Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ ambaye ameteuliwa kuwa msimamizi mkuu wa
uwakilishi kwa upande wa wasanii katika Tanzania kwanza nje ya Bunge maalum,
Muungano huo uko chini ya Mwenyekiti Augustino Matefu.
Akizungumza juzi na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam, Steve amesema kwamba ataungana na wasanii ambao
wako katika vyama mbalimbali kama vile Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, NCCR,
Mageuzi , Cuf na vyama vingine huku wote wakiwa na lengo moja tu la kuhimiza
mchakato wa katiba uendelee huku wanasiasa wakizingatia kudumisha amnai na
umoja wa Watanzania
Nyerere aliongeza kwa kusema kuwa
yeye hakuwa na kipingamizi pindi alipoambiwa amechaguliwa kuwa miongoni mwa
wasimamizi wa mpango huo ambao umewakutanisha vijana kutoka katika itikadi
mbalimbali za vyama vya siasa.
“Nilipoambiwa hili jambo niliweka
itikadi zangu za chama pembeni na kuuvaa Utanzania kwanza ili kuunganisha fani
zetu wote kwa pamoja na kuweza kuwahimiza wananchi wadumishe amani tuliyokuwa
nayo nchini” alisema Nyerere
Aliongeza pia kwa kuwaomba viongozi wa
dini masheikh na maaskofu wakiwemo mapadri wote kuungana nao wasanii hao katika
kuhimizaani ya amani ya nchi.
“Sisi wasanii tunapata riziki zetu
kutokana na amani na utulivu uliopo nchini mwetu hivyo kila msanii na
Mmtanzania aone ni jambo la fedheha kuiichezea amani ambapo siku ikipitea
tutakwenda kuomba hifadhi katika nchi za jirani zilizopata uhuru na kufuata
ushauri kutoka kwetu”.
Aliongeza kwa kusema kwamba ana
imani kubwa watanzania watawaelewa pindi watakapokuwa katika ziara hiyo
kuzunguka nchi nzima huku wakiwa na mabalozi watano kutoka kila nyanja ya sanaa
ambazo ni muziki wa taarab, Hip Hop, Sanaa za maigizo, Michezo na tamthilia.
Mkutano mkubwa unatarajiwa kufanyika Kibanda Maiti Zanzibar.
No comments:
Post a Comment