Mkuu wa husuma za kifedha kutoka tigo ANDREW HODGSON akizungumzia huduma hiyo mpya leo katika makao makuu ya tigo tanzania |
Kampuni ya simu za mkononi ya tigo Tanzania leo
imezindua huduma mpya ya kutuma na kupokea pesa ambayo ni ya kwanza Africa ya mashariki
itakayowezesha watumiaji wa simu za aina
ya ANDROID NA IOS nchini kutuma na kupokea fedha kwa njia rahisi na kwa ufanisi
zaidi.
Akizungumza na wanahabari leo makao makuu ya tigo
mkuu wa huduma za kifedha ANDREW HODGSON
amesema kuwa kuanzia sasa watumiaji wa simu za kisasa SMARTPHONES nchini
wataweza kufanya miamala yote ya tigo pesa kama kulipia huduma zote ,kulipa
fedha benk,na kuongeza salio kwa haraka na urahisi zaidi kwa kutumia tigo pesa
application.
Wanahabari wakisikiliza kwa makini leo |
Amesema kuwa kuanzia sasa wateja wa tigo wanaweza
kupata huduma zote za tigo pesa katika mtandao wa tigo bila kuingia gharama
yoyote ya data,wateja pia watakuwa na uwezo wa kutumia account zao za tigo pesa
popote pale walipo duniani kupitia internent ya wi-fi au mtandao wowote uliopo
wa internent kupitia simu ili mradi awe amesajiliwa na tigo pesa.
HODGSON amesema kuwa kupata huduma hii mpya ya tigo lazima uwe na simu ya kisasa yani smartphone ambayo inatumia program ya IOS au ANDROID.
No comments:
Post a Comment