.

HABARI ILIYOTIKISA JIJINI DAR LEO---UKAWA WACHARUKA---WASAMBAA KWENDA NCHI NZIMA KUANZIA KESHO KUTWA,NI MWENDO WA MAANDAMANO NA MIKUTANO,DK SLAA ASEMA KITAELEWEKA TU

Katibu mkuu wa CHADEMA dk WILBROAD SLAA akizungumza na wanahabari mapema leo juu ya ziara yao ya nchi nnzima

Umoja wa katiba ya watanzania UKAWA leo umejitokeza na kutangaza rasmi ratiba yao ya kuzunguka nchi nzima kwa lengo la kutoa elimu juu ya katiba mpya na mchakato huo ulipofikia
 
  Akizungumza na wanahabari ndani ya makao makuu ya CUF katibu mkuu wa CHADEMA dk WILBROD SLAA amesema kuwa ukawa sasa imeanza rasmi kufanya maandamano na mikutano nchi nzima kila kona ya Tanzania kwa lengo la kuwafikia wananchi na kuwaeleza ukweli kuhusu mchakato wa katiba 
Katibu mkuu wa NCCR mageuzi MOSENA NYAMBABE akizungumza ambaye ni mmoja kati ya viongozi wa ukawa ambao watazunguka nchi nzima

Dk SLAA anasema kuwa kwa wale ambao wanasema kuwa UKAWA ni nguvu ya soda wanapotea kwani muungano huo haujaja kwa bahati mbaya kwani wamejipanga kuhakikisha kuwa inawaleza watanzania ukweli juu ya katiba na jinsi chama cha mapinduzai CCM wanavyoupotosha umma juu ya mchakato huo.

  Aidha dk SLAA amesema kuwa  kauli ambazo zilitolewa na viongozi wa juu wa chama cha mapinduzi CCM kuwa Tanzania haiitaji sana katiba mpya ni kauli za mtu ambaye hajafika darasani na ni kuwapotosha watanzania na kauli hizo zinatakiwa kupigwa vita sana kwani zinaupotosha umma.
JULIUS MTATIRO akizungumza
Wanahabari mbalimbali wakiwa wanasikiliza kwa makini mkutano huo wa ukawa na wanahabari
UKAWA wametangaza kufanya maandamano na mikutano kona zote za Tanzania kwa kuigawa Tanzania kwa kanda tatu ambazo ni KANDA YA KATI,KANDA YA KASKAZINI,NA NYANDA ZA JUU KUSINI,ambapo viongozi kutoka vyama vitatu wakiwemo makatibu wakuu wote wataongoza mikutano hiyo ambayo itaanza rasmi tarehe 14 mwezi huu.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.