Tuesday, June 24, 2014

BREAKING NEWZZ---SAKATA LA KUTEKWA NA KUTESWA KWA RAIS WA WANAFUNZI BUGANDO,MTANDAO WA WANAFUNZI WATOA TAMKO KALI,WATUPA LAWAMA KWA POLISI.SOMA TAMKO LOTE HAPA

Mwenyekiti  wa Mtandao Alphonce  Msako akizungumza na wanahabari muda mchache uliopita jijini Dar es salaam
N a Karoli Vinsent


     HUKU wingu zito likiwa bado limetanda,kuhusu kutekwa na kuteswa kwa Rais wa chuo kikuu cha Sayansi ya afya BUGANDO mkoani Mwanza Mussa Mdede,Nao mtandao  wa Wanafunzi nchini “TSNP”umelivaa jeshi la Polisi nchini na kusema bado limeshindwa kuzuia  vitendo hivyo vya kinyama.

     Kauli, hiyo imetolewa leo Jijin Dar es Salaam na Mwenyekiti  wa Mtandao Alphonce  Msako,wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari ambapo alisema wao wamesikitisha na vitendo vya kinyama alivyofanyiwa Rais wa  chuo Bungando na kulitaka Jeshi la polisi kuacha kukaa kimya kwenye suala hilo.

     “Sisi viongozi wa mtandao huu  wanafunzi “TSNP” tumezipokea taarifa hizi kwa mshtuko mkubwa sana juu ya tukio la kutekwa na kuteswa kwa mwanafunzi huyo,mtandao huu unaamini kwamba mazingira ya utekwa ji nyara yalifanyika ni dhahiri”


    “Kwamba wahusika ni watu wenye utaaluma mkubwa ,na tunashangaa  hakuna taarifa rasmi kutoka Jeshi la polisi nchini,kwa hali hii inatupa shinda sana sisi wanafunzi kuhusu ulinzi wetu kwenye vitendo hivi vya utekaji”alisema Msako.

      Msako,alizidi kusema ukimya huu wa jeshi la polisi ,ndio unafanya vitendo hivi vya kinyama kwa wanafunzi kuzidi kushika kasi katika maeneo ya vyuo vikuu,lakini mpaka sasa hakuna wahusika wowote waliokamatwa.

     “Tunashangaa sana,kwani hivi karibuni kumeibuka vitendo vya kinyama wanavyofanyiwa wanafunzi wa Vyuo vikuu,kwamba wanatekwa,kupigwa risasi na kuporwa lakini hakuna mtu yeyote aliyekamatwa wala jeshi la polisi kuonyesha ushirikiano”alizidi kusema Msako.

      Msako,ambaye ni mwanafunzi kutoka chuo Kikuu huria,aliwataka wanafunzi nchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu,na kuwataka kuwa wapole ambapo Jeshi la polisi likifanya uchunguzi suala hilo.
Katika Hatua Nyingine Mwenyekiti huyo,alilitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu matukio ya utekaji ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara hapa nchini.

       Ikumbukwe Tamko la Mtandao huu wa wanafunzi nchini “TSNP”imekuja siku moja tu kupita Baada Rais huyo wa Serikali ya Wanafunzi chuo kikuu  cha Sayansi ya Afya na tiba Bugando”Cuhas” mkoani mwanza Mussa Mdee ambaye anadaiwa kutekwa nyara ambapo alipatikana akiwa hajitambaina mwenye uchovu mwingi.

No comments: