Jeshi la Polisi Kanda
Maalum Dar es Salaam limetangaza msako mkali wa kuwatafuta na kisha kuwakamata
wale wote waliohusika katika tukio la kuuawa kwa kupigwa risasi kwa MTAWA wa
Kanisa Katoliki Sista CRESENCIA D/O KAPURI, miaka 50, mhasibu Parokia ya Kanisa
Katoriki Makoka, lililotokea tarehe
23/06/2014 eneo la Ubungo Kibangu.
Awali, marehemu akiwa
ameongozana na wenzake ambao ni Sista BRIGITA D/O MBAGA, Miaka 32, Mkazi wa
Makoka pamoja na dereva wao MARK S/O PATRICK MWARABU akiendesha gari aina ya
T/Hilux PICK-UP namba T213 CJZ wakitokea benki ya CRDB tawi la Mlimani City,
walipofika eneo la Ubungo Kibangu ili kulipa deni la chakula katika duka la
bwana THOMAS S/O FRANCIS ndipo walipotokea majambazi wawili wakiwa na pikipiki
ambayo haikusomeka namba na mmoja akiwa na bunduki aina ya SMG wakampiga risasi
ya kidole gumba cha mkono wa kulia dereva wa gari hilo kisha kupiga mtawa huyo
risasi ya kifuani na kupora mkoba uliokuwa na pesa kiasi cha Tshs: 20,000,000/=
(million ishirini) na nyaraka mbalimbali za ofisi.
Kufuatia tukio hilo
Jeshi la Polisi limeazimia kufanya yafuatayo:
·
Kwanza limegundua kwamba matukio ya
ujambazi hasa unaohusian na wananchi kuporwa kiasi kikubwa cha pesa unaanzia
katika mabenki ambapo majambazi huwafuatilia wateja waingiapo au kutoka katika
benki mbalimbali.
· Imeonekana kwamba mara nyingi mabenki
yanapohitahi kusafirisha pesa nyingi hutumia escort ama ya Polisi au taasisi
nyingine zinazotoa huduma ya ulinzi.
· Ni muhimu kwa mabenki kuwahimiza wateja
wao kutochukua kiasi kikubwa cha pesa kiholela kwani ni rahisi kuporwa na watu
wasio na nia njema
·
Aidha mabenki yawahimize wateja wake
kutumia njia mbadala za kusafirisha pesa nyingi kama vile matumizi “CHEQUE”,
Kufanya miamala bila kadi (Cardless transactions), matumizi ya kadi za ATM, na
njia nyinginezo za kifedha.
·
Jeshi la Polisi linawahimiza mameneja wa
benki zote kutoa taarifa polisi endapo kuna mteja yeyote atakaidi ushauri wa
taasisi za fedha. Aidha benki ziwe na kitego
Pia, tunawaomba
wananchi watoe ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za
kutosha ili kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa wa ujambazi ili sheria iweze
kuchukua mkondo wake. Pia wafanyabiashara na taasisi nao na wasitumie njia za
mkato kwa faida ya ulinzi wa maisha na mali zao. Aidha, benki ziwe na kitengo
cha ushauri wa usalama wa wateja. Ni muhimu watumie mitandao ya usafirishaji
fedha ambayo ni salama kama vile M-PESA, AIRTEL Money, TIGO Pesa, Easy Pesa,
nk.
No comments:
Post a Comment