Wednesday, June 25, 2014

HII NDIO TAARIFA RASMI KUHUSU HABARI YA KIFO CHA MH SHUKURU KAWAMBWA


Kutokana na baadhi ya mitandao ya kuijamii muda mchache uliopita kuandika habatri juu ya kumuhusisha na kifo mbunge Shukuru kawambwa mtandao huu umezungumza na watu wa karibu wa waziri huyo na kudai kuwa shukuru kawambwa ni mzima wa afya na habari zinazoenea ni uzushi mkubwa na hazina ukweli wowote.

           Na hii ndio mesege kutoka Kwa mbunge RIDHIWAN KIKWETE juu ya uvumi huo.

    Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na habari zinazoenezwa Mitandaoni kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza.

                UKWELI
        Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.
Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mnec)
Mbunge -Chalinze


No comments: