Profesa LIPUMBA akipongezwa na aliyekuwa mpinzani wake katika uchaguzi huo baada ya matokeo kutangazwa muda huu hapa katika ukumbi wa ubungo plaza jijini Dar es salaam |
Uchaguzi mkuu wa cjhama cha wananchi CUF umemalizika hapa jijini dar es salaam ambapo aliyekuwa mwenyekiti profesa IBRAHIM HARUNA LIPUMBA amechaguliwa tena kukiongoza chama hicho kwa miaka mingine mitano baada ya kupata kura 659 kati yakura 689 zilizopigwa ambapo ni ushindi wa zaidi ya 95% ya kura zote ambapo aliyekuwa mpinzani wake pekee katika uchaguzi huo mh CHIEF YEMBA amepata kura 30 sawa na aslimia 4.3% ya kura zote zilizopigwa.
Katika nafasi ya makamu mwenyekiti mgombea alikuwa mmoja ambaye ni JUMA DUNI HAJI ambaye katika kura 667 zilizopigwa amepata 662 sawa na aslimia 99.25 ya kura zote na kutangazwa rasmi kuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho.
Aidha katika nafasi ya katibu mkuu wa chama hicho kama kawaida mgombea alikuwa mmoja ambaye ni MH SEIF SHARIF HAMAD ambaye katika kura 678 zilizopigwa amejinyakulia kura 675 sawa na aslimia 99.5% ya kura zote zilizopigwa hivyo kutangazwa rasmi kuwa katibu mkuu wa chama hicho akiendelea kushika nafasi aliyokuwa anaiongoza.
Sura za furaha baada ya kurudi tena katika madaraka yao waliyokuwa nayo hapo awali kabla ya mchakato wa uchaguzi |
No comments:
Post a Comment