Monday, June 16, 2014

HOT NEWZZ--SIKU YA MTOTO WA AFRICA,LHRC WASEMA BADO MTOTO WA KITANZANIA ANAKUMBWA NA CHANGAMOTO NYINGI,WAIKUMBUSHA SERIKALI KUWAJALI WATOTO

Kaimu mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC  Bw HAROLD SUNGUSIA akizungumza na wanahabari muda mchache uliopita
 Ikiwa leo bara la Africa linaadhimisha siku ya mtoto wa Africa kituo cha Sheria na Haki za binadamu Tanzania LHRC kimesema kuwa bado serikali ya Tanzania haijaonyesha dhamira ya dhati katika kulinda na kuheshimu haki za mtoto wa kitanzania kama ilivyo katika mataifa mengine .

   Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu bw HAROLD SUNGUSIA wakati wa mkutano na wanahabari alipokiwa akitoa tamko la kituo hicho juu ya siku hii ya mtoto wa Africa ambapo amesema kuwa pamoja na jitihada zilizofanywa na serikali ikiwemo kuundwa kwa sheria ya mtoto ya mwaka 2009 na kuridhia mikataba mbambali  ya kimataifa bado mtoto wa kitanzania anakabiliwa na changamoto nyingi ambazo bado serikali imeshindwa kuzitatua.

Akitaja matukio ambayo mablimbali ya ukiukwaji wa haki za mtoto ambayo yanamkuta mtoto wa kitanzania amesema kuwa matukio kama ,kubaguliwa,kunyanyapaliwa,kubakwa,kulawitiwa,kudharauliwa,kufanyishwa kazi za ndani,na kunyanyaswa,pamoja na tabia ya wazazi kuwatuma watoto  wao vileo mbalimbali ni matukio machache ambayo bado yanamtokea mtoto wa kitanzania huku serikali ikishindwa kuyamaliza matatizo hayo.

Bw SUNGUSIA ametolea mfano tatizo la kulawitiwa ambapo amesema kuwa kwa mwaka jana tu watoto zaidi ya mia nane walirepotiwa kulawitiwa idadi ambayo ni kubwa sana kwa nchi kama Tanzania,huku akiitaka serikali kuhakikisha inalivalia njuga swala hilo kwani limeanza kuota mizizi.
Wanahabari wakiwa makini kumsikilza
Aidha kituo cha sheria na haki za binadamu wamesema kwa kuheshimu umuhimu wa mtoto katika bara letu la Africa na nchi yetu ni lazima kuheshimu na kuzingatia sheria za nchi zinazomlinda mtoto,elimu ya haki ya mtoto itolewe pamoja na kila mtu kuwajibika katika kumlinda mtoto katika kuhakikisha uhuru wa mtoto unapatikana.


   Siku ya mtoto wa Africa inaadhimisha kila siku  barani Africa kuwakumbuka watoto waliouawa huko Africa ya kusini wakiwa katika maandamano ya kudai haki na usawa wa elimu katika kitongoji cha Soweto mwaka 1976

No comments: