SAKATA linalohusu kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), limechukua sura mpya baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kuwashambulia kwa maneno makali, wabunge wawili Zitto Kabwe wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) na David Kafulila wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi).
HABARI24 likuwapo wakati Maswi akitumia maneno makali kwa kuyarudia, akikejeli nyaraka zinazotajwa kuwa ni ushahidi wa jinsi IPTL ilivyouza hisa zake na fedha kutolewa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika akaunti maalumu ya pamoja (Escrow), akisema nyaraka hizo ni karatasi za kufungia vitumbua zinazosambazwa na wabunge hao aliowaita “washenzi”.
Kauli hiyo ya Maswi imekuja siku mbili tu baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema kushambuliana na Kafulila kwa maneno makali malumbano yao yakianzia ndani ya Bunge na kuendelea walipotoka, kila mmoja akiamini kauli aliyoitoa ilikuwa ni sahihi.
Werema alimfananisha Kafulila na tumbili na yeye kumuita mwanasheria huyo mwizi. Tumbili ni mnyama wa porini wakati mwizi ni mtu anayetenda uhalifu kwa kuchukua kitu au mali isiyo yako.
No comments:
Post a Comment