Friday, June 27, 2014

PATA NAFASI YA KUSOMA KAULI TANO KALI ALIZOZUNGUMZA KOCHA MPYA WA YANGA MAXIMO MBELE YA WANAHABARI LEO

Kocha MAXIMO akizungumza na wanahabari makao makuu ya timu hiyo jijini Dar es salaam
Kocha mpya wa timu ya yanga ya dar es salaam mbarazili MARCIO MAXIMO leo amezungumza na wanahabari kwa mara ya kwanza jijini dar es salaam ambapo katika mambo mengi aliyoyazungumza ameonekana kuwaahidi mambo makubwa mashabiki wa timu ta yanga.

Naomba ninukuu kauli zake tano ambazo amezitoa na zikaonekana kuwafurahisha wapenzi wa timu ya yanga na viongozi wake 

1-Nimekuja kuifanya timu ya yanga kuwa kama timu ta TP MAZEMBE ya congo,nadhani nina uwezo huo na nadhani kwa kushirikiana na viongozi wa timu hii tutaweza.

2-Nataka kuipeleka yanga level za kimataifa zaidi tofauti na sasa

3-Nataka kutengeneza timu ya yanga kuwa timu yenye upinzani mkubwa tanzania na barani africa kwa ujumla

4-Nataka kuifanya yanga iwe timu yenye mvuto na ifike kipindi timu hii wazungu na wachezaji wa kutoka ulaya kuja kucheza hapa yanga na kwa kuanza hilo naanza kwa kumleta mchezaji mzuri toka Brazil anaitwa ANDERY CONTINYO ambaye atawasili leo jioni.

5-Swala la kaseja ni kwamba sina bifu na kipa wa yanga JUMA KASEJA nampenda sana yaliyopita yamepita sasa tugange yajayo tuwaze kuijenga timu yetu.

MAXIMO ATAKUWA AKIJIZOLEA KITITA CHA MILION 19 KWA MWEZI AKIWA YANGA

No comments: