Tuesday, June 10, 2014

MBOWE ZIARANI JIMBONI KWAKE,PICHA MBILI HIZI HAPA

Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe akiwa pamoja na Kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDF), wakikagua Dara la Marire, Iwala, ikiwa ni sehemu ya ziara anayofanya kwa ajili ya kufanya tathmini ya miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo ambayo inahitaji kupata msukumo wa kuongezewa nguvu za ujenzi na mfuko huo ambao yeye ni mwenyekiti wake.

Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe akiwa ameongozana na Kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDF) wakikagua moja ya jengo linalopaswa kuwa nyumba ya walimu katika Shule ya Msingi Tindigani, ikiwa ni sehemu ya ziara kwa ajili ya kufanya tathmini ya mahitaji katika miradi mbalimbali ya maendeleo inayohitaji kuongezewa msukumo na mfuko huo ambao yeye ni mwenyekiti wake.

No comments: