Tuesday, June 10, 2014

EXCLUSIVE--BAADA YA KESI DHIDI YA WAZIRI MKUU PINDA KUTUPILIWA MBALI,WALIOMSHTAKI WAIBUKA TENA,SOMA WALICHOKISEMA HAPA


Makamu mwenyekiti wa chama cha wanasheria wa Tanganyika TLS  FLAVIANA CHARLES akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam mapema leo juu ya kesi hiyo
           Baada ya kesi iliyokuwa imefunguliwa katika mahakama kuu ya Tanzania dhidi ya waziri mkuu wa Tanzania MIZENGO PINDA kutupiliwa mbali na mahakama hiyo mapema wiki jana,chama cha wanasheria Tanganyika TLS pamoja na kituo cha sheria na haki za binadamu  LHRC ambao ndio waliomshtaki waziri mkuu  leo wametoa tamko lao juu ya kufutwa kwa kesi hiyo huku wakitangaza kurudi tena mahakamani kupinga baadhi ya vipengele kwenye hukumu hiyo,
Wanasheria hao wakiwa wanatoa tamko lao
           Akizungumza na wanahabari makamu mwenyekiti wa chama cha wanasheria wa Tanganyika Bi FLAVIANA  CHARLES  amesema kuwa kimsingi wamepokea uamuzi huo wa mahakama na kuridhika na tafsiri ya mahakama kuhusu ibara ya 100(2) kwamba kinga ya wabunge ina  \ mipaka na ukomo kisheria na inapashwa kuzingatia katiba na sheria nyingine nchini,hivyo kinga hiyo inaweza kuhijojiwa mahakamani ambapo amesema kuwa hilo ni jambo muhimu sana ambalo litasaidia kujenga misingi ya kuheshimu haki za binadamu na utawala wa kisheria na utawala bora.
MPALE MPOKI ambaye ndiye kiongozi wa Mawakili hao waliofungua kesi hiyo

Wakili PETER KIBATALA akizungumza na wanahabari katika mkutano huo
        Aidha wanasheria hao wamesema kuwa hawajaridhika na kipengele kilichopo katika hukumu hiyo ambacho kinasema kuwa kituo cha sheria na haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kuwa ni mashirika na sio watu binafsi na hawakuwa na uwezo wa wa kisheria wa kufungua shauri hilo makahakamani kwa kuwa kauli za waziri mkuu hazingeweza kuwaadhiri wao moja kwa moja,kauli ambayo wanasheria hao wameipInga na kuahidi kurudi mahakamani kukata rufaa juu ya kipengele hicho na kuiomba mahakama itengue kipengele hicho.
Kaimu mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC  HAROLD SUNGUSIA akizungumza
       Kesi dhidi ya waziri mkuu ilifunguliwa mnamo Augost 1 mwaka 2013 katika mahakama kuu ya Tanzania kupinga kauli zake alizozitoa bungeni mnamo tarehe 20 mwezi wa 6,2013 alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo ambapo aliwataka polisi kuchukua hatua ya kupiga watu endepo watafanya fujo kama tunavyoinukuu hapo chini.

“UKIFANYA  FUJO, UMEAMBIWA  USIFANYE  HIKI  UKAAMUA WEWE  KUKAIDI  UTAPIGWA  TU,EEH MAANA HAKUNA  NAMNA  NYINGINE, EEH  MAANA  LAZIMA TUKUBALIANE  KUWA  NCHI  HII TUNAIENDESHA  KWA MISINGI YA KISHERIA,SASA KAMA WEWE UMEKAIDI HUTAKI,UNAONA KWAMBA NI IMARA ZAIDI,WEWE NDIO JEURI ZAIDI,WATAKUPIGA TU,NA MIMI NASEMA WAWAPIGE TU,KWA SABABU HAKUNA NAMNA NYINGINE,EEH  MAANA  TUMECHOKA SASA".


No comments: