Badhi ya wasichana kutoka shule mbalimbali jijini dar es salaam wakiwa katika mafunzo hayo |
Wasichana nchini Tanzania wamepewa changamoto ya
kujiendeleza katika masomo ya technohama ili kuweza kuongeza upeo wao katika
matumizi ya computer na kuweza kuchangia katika maendeleo ya kijamii kwa ujumla
nchini Tanzania.
Changamoto hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na meneja
wa uwajibikaji kwa jamii kutoka kampuni ya tigo Tanzania Bi WOINDE SHISAEL
wakati akizungumza na wanafunzi wa kike wapatao 100 kutoka shule za secondary
mbalimbali waliokuwa katika mafunzo maalum ya technohama yaliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali
linalijihusisha na technohama APPS AND GIRLS ambao pia ni mmoja wa washindi wa
program maalum ya wajasiriamali wa kijamii TIGO REACH FOR CHANGE
Bi WOINDE amesema kuwa “mkakati wa huduma ya
uwajibikaji walionao tigo ni kuwezesha jamii kupitia matumizi ya vyombo vya
kidigital” ambapo ametoa rai kwa wanawake na wasichana wote kujitokeza zaidi
kujiendeleza kidigital kupitia technohama huku akiongeza kuwa ni dhana potofu
kuwa wasichana hawawezi kufanya vizuri katika technohama wakati wana nafasi
kubwa sana.
Aidha amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga wasichana
tu kwa sababu wanawake wengi wameonekana kuwa nyuma sana katika kujihusisha
katika technohama.
Meneja wa uwajibikaji kwa jamii kutoka kampuni ya tigo Tanzania Bi WOINDE SHISAEL |
Muasisi wa APPS AND GIRLS bi CAROLYNE EKYARISIIMA |
Naye muasisi wa APPS AND GIRLS bi CAROLYNE EKYARISIIMA ampaye pia ni mmoja wa washindi wa
dola 25,000 za kimarekani kutoka tigo reach for change kwa mwaka huu amesema
kuwa mafunzo haya yanazingatia kwapatia wasichana utaalam katika kutengeneza
tovuti kama njia moja wapo ya kuwahamasisha katika maswala ya technohama.
Shule zilizohudhuria mafunzo hayo ni pamoja na
kisutu,jangwani,na kibasila ambapo mafunzo hayo ni ya simku moja.
No comments:
Post a Comment