Wednesday, June 11, 2014

UCHUNGUZI KAMILI--LIJUE KUNDI MPYA NDANI YA CCM NI "THREE MAN"WAPANIA KUMZIMA LOWASA NA KUMSIMAMISHA MGOMBEA WAO,


Na Karoli Vinsent

         KATIKA kile  kinachotafsiriwa  huwenda  chama cha Mapinduzi CCM kikapasuka Vipande vipande kwenye uchaguzi Mkuu Mwakani zimeanza kuonekana,Baada ya Makundi yanoyosaka Urais kuzidi kuongekeza, mtandao huu umebaini.

Makundi hayo,ambayo yameapa kutumia kila njia kuhakikisha yanamtoa mtu wao mmoja kuja kumrithi Rais anayemaliza mda wake  Jakaya Kikwete,hivi sasa limeibuka kundi jengine ambalo limepanga kuhakikisha mmoja wao anakamata nafasi hiyo ya Juu ya nchi.

         Kundi hilo jipya liloibuka ambalo linajiita kwa kingereza “three man”yaani wanaume watatu, ambao ni aliyekuwaWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba pamoja na aliyekuwa waziri wa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja.


         Kundi hilo ni jipya limeibuka ikiwa miezi michache baada  chama cha Mapinduzi CCM,ikiwa  tayali imewafungia Makada ambao walianza kuonyesha dalili  za kutaka Urais ndani ya chama hicho kwenye uchaguzi Mkuu mwakani,

        Makada hao ni pamoja Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond,  ambaye pia ni Mbunge wa Monduli,Edward Lowassa,  wengine ni Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye pamoja na aliyepata kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja,January Makamba,Samweli Sitta,ambao wote kwa pamoja wanatumikia kifungo cha miezi 12 kutofanya kampeni za kusaka urais.

   Kundi hilo jipya limejipanga kuhakikisha linatumia ushawishi walikuwa nao ndani ya Halmashauri kuu Chama cha Mapinduzi NEC ,na kwa wananchi vilevile  kuhakikisha wanaipunguza kasi ya waziri mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa,ambaye anaonekana kuwa mwiba mkali ndani ya chama hicho kikongwe barani Afrika.

       Naye mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi NEC kutoka mikoa ya Nyanda za juu kusini aliyezungumza na Mwandishi wa Mtandao huu ambaye hakutaka Jina lake liandikwe kwenye mtandao huu alisema Chama chake kinaelekea kubaya kutakana na kila mtu kutaka urais.

        “Yaani hizo taarfa mimi mwenyenyewe nimezisikia kwamba limeundwa kundi jipya linalojiita “three man” eti nalo linataka kumtoa mtu miongoni mwao ili achukue Urais kwenye uchanguzi mkuu mwakani hivi jamani akuna vitu vyengine vya kufikilia mpaka urais”

      “Nchi leo inamatatizo lukuki serikali haina pesa na bajeti inasuasua huko bungeni,leo viongozi wanafikiria urais,na mimi naona kuna ishara mbaya sana chama hichi kupagalanyika mwakani na  sababu itakayosabisha ni hawa wasaka urais”alisema Mjumbe huyo

       Duru za kisiasa zinasema kuongezeka makundi ya chama hicho zinaashiria Mpasuko mkubwa ambao utakitikisa chama hicho ambacho ni Kikongwe ambacho kipo madarakani,na mpasuko huo ambao haujawahi  kutokea tangu chama hicho kianzishwe.

        Kwa upande wake Kigogo kutoka ndani wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM, UVCCM,aliyezungumza na mwandishi wa mtandao huu kwa sharti la kutoandikwa jina lake mtandaoni, alisema makundi hayo yanayozidi kuibuka kwenye chama hicho ni njama zinazofanywa ili kumpoteza kabisa Waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa.

      “Hizo njama tu ndugu yangu ambazo zinafanywa na watu wasiomtaka Edward Lowassa kushika nafasi ya Urais ndio maana wanajifanya kuanzisha makundi mapya ili kumzima kabisa mzee Lowassa”

       “Na sisi vijana tunajua kwamba makundi hayo yanaanzishwa ili kumzima lowassa,nakuhakishia kaka sisi hatutakubali na tuko tayari kukihama hata chama chenyewe kama endapo jina la Lowassa kama litakatwa  pale NEC”alisema Kigogo huyo kutoka UVCCM

       Naye mchambuzi na Msomi wa Masuala ya Siasa kutoka Chuo kikuu cha Dodoma Seiph Yahaya ,alisema chama cha mapinduzi kingojee kupasuka,kutokana na Chama hicho kutumia njia mbaya kumzima Lowassa katika harakati zake za kutaka Urais.

       “Hivi nani asiyejua kwamba ule mpango wa kuwakataza bodaboda kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam ni miongoni mwa mikakati ya kumpotezea sifa mzee wetu Lowassa,kwani hata hiyo sheria wanayoisema kwamba hao bodaboda kuingia katikati ya jiji,imetungwa lini si zaidi ya miaka miaka saba nyuma”

        “Kwanini waianze kuitekeleza leo baada ya Edward Lowassa kuzindua “Saccos” ya hao bodaboda ambayo iliyompa umaarufu sana jiji humo,sasa wamezikataza pikipiki  hizo,na sasa siwezi kushangaa hata makundi mapya yaibuke tunajua tu wanataka kumzima kiongozi huyo”alisema Seiph Yahaya.


No comments: