Monday, July 21, 2014

exclusive --MIAKA MIWILI YA KUFUNGIWA KWA MWANAHALISI-SOMA KILICHOTOKEA


Na Karoli Vinsent

         KATIKA kujali ubora wa Gazeti la Mwanahalisi mtandao huu,unakuleta simulizi kuhusu sakata la kufungiwa Gazeti hilo,ambapo gazeti hilo limefungiwa kwa mda usiojulikana na Serikali kutokana na Habari zake zilizokuwa zikiandikwa.

        Gazeti la mwanahalisi lilifungiwa Tarehe 30/07/2012 na Waziri wa  Habari ,vijana utamaduni na Michezo   Dkt. Fenella Mukangara ambapo alitoa Hukumu ya kulifungia kwa muda usiojulikana kwa kile alichokiita kwamba mwenendo wa Gazeti hilo si mzuri,kwani limekuwa likiandika Makala zenye uchochezi na kuleta Uhasama  na uzushi na kupelekea wananchi kukosa Imani na Vyombo vya Dola hali inayoweza kuhatalisha Amani ya nchi.



         Ambapo, waziri huyo alitumia Sheria Kandamizi ya Magazeti ya Mwaka 1976,kifungu Namba,25 ambayo inampa Mamlaka waziri anae husika na masuala ya Habari, kulifungia Gazeti lolote pale yeye mwenyewe anaona kwa mawazo yake kwamba Gazeti linakiuka sheria ya nchi.

        Adhabu hiyo ilianza kutumika kwanzia Tarehe 30 mwezi Julai mwaka 2012,ambapo katika adhabu hiyo ilisema kwanzia sasa gazeti hilo limefungiwa kwa mda usiojulikana.

       Kwa sasa Gazeti hilo limetimiza Miaka miwili tangu lifungiwe lakini bado hakuna nia ya dhati kutoka kwa Serikali katika kulegeza Adhabu hiyo kubwa kwenye historia ya Magazeti nchini, huku serikali ikijua kwamba Nchi yetu Tanzania iko kwenye ,Mfumo wa Kidemokrasia ambao unatoa mwanya kwa Mtu kujieleza,

      Vilevile Serikali imeshindwa hata kutambua kwamba ndani ya Katiba ya nchi  Ibara ya 18 ambayo inatoa uhuru wa kujieleza kwa kila mtu.
      Mtandao huu utakuletea Mikingano ambayo imeibuka baada ya Gazeti hilo kufungiwa kutoka Kwa Viongozi,ambapo malamala kwa mala wamekuwa wakitofautiana kuhusu kufungiwa gazeti hilo ambalo lilibeba Taswira ya ukombozi katika fani hii ya Habari.
Gazet la Mwanahalisi lilianzishwa  miaka mitano iliyopita na kuwa chini ya Kampuni ya Halihalisi Publishers Ltd,ambapo mkurugenzi wa Kampuni hiyo alikuwa ni Said Kubenea.

          Vilevile Kubenea ambaye ni miongoni mwa Waandishi bora wanofanya Habari za uchunguzi nchini,ambaye alikuwa anafuata nyayo za Mwandishi wa Zamani Gazeti la Mfanyakazi Stani Katabalo,ambaye naye alikuwa ni Miongoni mwa Waandishi wanaofanya na Kuandika Habari za Uchunguzi nchini katika kipindi hiko cha nyuma.

        Licha ya Kubenea  kuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Halihalisi pia alikuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo la Mwanahalisi.

          Katika Kazi za Hatari za kufanya Habari za Uchunguzi Saed Kubenea aliwai kukumbana na Matatizo ikiwemo kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikana na kupelekea kwenda kutibiwa nje ya nchi ili kuweza kuoka Macho yake ambayo yalidhulika kwa Tindi kali hiyo aliyokuwa amemwagiwa Usoni hususani kwenye Macho.

        Lakini mpaka sasa Jeshi la Polisi halijawai kuwataja wala kuwakamata watu waliohusika na kumfanyia Vitendo hivyo vya kinyama mwandishi huyo nguli katika fani ya Habari nchini.
Gazeti hilo ambalo lilikuwa lilikuwa likifichua mambo ya mabaya yaliyokuwa yakifanywa na Serikali,wanasiasa pamoja Viongozi wa Mashirika mbalimbali hapa nchini,

        Hii ni sehemu ya kwanza ya Sakata la kufungiwa Gazeti hili la mwanahalisi,usikose tena kesho kujua mengine kuhusu gazeti hilo,ambapo Mtandao huu utakuletea Simulizi ndefu kwanzia leo tarehe 21 hadi tarehe 25 mwezi siku ambayo ndio tarehe ya mwisho kuchapisha Gazeti,Nia yetu ni  tunataka  umma ujue na kufahamu ukweli ulioko kwenye Sakata la Gazeti hili na Sababu iliyopeleka kufungiwa Gazeti hili,



     Tunafanya hivi labda serikali yetu inaweza kubadilisha mawazo na kuweza kulifungulia Gazeti hilo ambalo lilikuwa limetoa ajira kwa watanzania wengi hapa nchini.  


No comments: