Saturday, July 19, 2014

HABARI KUBWA LEO--HAWA NDIO VIONGOZI WA CHADEMA KIGOMA WALIOJIVUA UONGOZI LEO NA KUJIUNGA NA CHAMA KIPYA CHA ACT

???????????????????????????????
Viongozi wa CHADEMA Mkoa waliojiuzuru ,kuoka kushoto ni Msafi Wamarwa aliyekuwa Katibu wa chama Mkoa,wakatika ni Ramadhani Kasisiko aliye kuwa Mwenyekiti wa chama Mkoa pamoja Malumba Simba liyekuwa katibu wa BAWACHA

VIONGOZI wa chama cha maendeleo na demokrasia (CHADEMA)wajeuzuru leo rasmi nyadhifa zao pamoja na uanachama wa chama hicho.
Viongozi hao waliotangaza kujiuzuru nafasi zao katika chama hicho mbele ya waandishi wa habari ni Jafari Ramadhani Kasisiko ambaye alikuwa Mwenyekiti wa chama Mkoa,Msafiri Hussen Wamarwa amabye alikuwa katibu wa chama Mkoa pamoja na Malunga Masoud Simba alikuwa Kaibu wa Baraza la wanawake BAWACHA.

Akiangaza uamuzi kwa niaba ya wenzake aliyekuwa Mwemnyekii wa CHADEMA Jafari Kasisiko alisema kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kuona CHADEMA kimepoeza sifa ya kuwa chama cha demokrasia na kuwa chama cha wababe.
”Sifa iliyokuwa inaufanya ubaki CHADEMA ni kwakuwa kilikuwa ni chama cha dempkrasia lakini hivi sasa kimeshapoteza hiyo sifa na kuwa chama cha kibabe na kinachokiunga misingi ya demokrasia hatuna sababu ya kuendelea kubaki katika chama hiki”alisema Kasisiko
Kasisiko ambaye aliondoka chama cha CCM mwaka 1985 na kukaa nje ya siasa kwa muda kabla ya kujiunga na CHADEMA mwaka 1994.
”Kwa mfano wa demokrasia inayokiukwa CHADEMA kipindi kile aliyekuwa Naibu katibu Mkuu wa CHADEMA Mhe Zitto alipoaka kugombea nafasi ya unyekii CHADEMA livuliwa wadhifa wake baada ya kufuaia kutangaza nia sasa pale Zitto kosa lake nini?alihojilakini ukipiia kaiba ya CHADEMA hakuna sehemu inayokaza mwananchama kugombea nafasi ya unyekii”
”Kwahiyo katika CHADEMA sasa hivi nafasi ya unyekiti ni kiu nyeti sana hastahili mwanachama yeyote kugombea”alisema Kasisiko
Alisema kuwa pamoja na kuwa wamechukua muda mrefu kabla ya kuangaza uamuzi wao huo walikuwa na sabbabu za msingi zilikuwa zinawafanya wasiangaze haraka uamuzi huo,lakini tangu Zitto alivyovuliwa madaraka yake walikuwa hawana imani tena na chama kwasababu hawezi kuwa ndani ya chama ambacho ni mamlaka ya fulani.
Naye aliyekuwa Katibu wa Mkoa wa chama hicho Msafiri Wamarwa alisema kuwa kwa ridhaa yake toka moyoni bila ya kushawishiwa na mtu ameamua kuondoka CHADEMA na kabla ya uamuzi huo alikaa chini na kutafakari sana na kuona njia sahihi ni kutoka CHADEMA kwakuwa chama hicho hakina faida kwa wananchi.
 Baada ya kujiuzuru uongozi na uanachama toka CHADEMA aliyekuwa Mwenyekii wa chama hicho Mkoa Ramadhani Kasisiko anajiunga na chama kipya cha cha siasa cha Allience  for Change  and Trasparency(ACT)lakini wenzake wamesema bado wanaafuta chama makini cha kujiunga nacho.

No comments: