Thursday, July 24, 2014

HILI NDILO ALILOLIFANYA PETER MSIGWA JIMBONI KWAKE LEO

SAM_6953
Baadhi ya misaada iliyotolewa na mbunge wa Iringa mjini Mch. Peter Msigwa kwa kituo cha
chuo cha Kitanzani Islamic center kilichoko mjini Iringa.
SAM_6980
Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa akikabidhi msaada wa Sukari, kwa Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Abubakari Chalamila kwa ajili ya kituo cha Kitanzani Islamic Center kilichoko mjini Iringa.
…………………………………………………………………………………

Na Denis Mlowe,Iringa
MBUNGE wa Iringa Mjini(Chadema) Mchungaji Peter Msigwa amekikabidhi chuo cha Kitanzani Islamic Center msaada wa Sukari,Unga wa Ngano, tende na mafuta ya kupikia ikiwa ni utaratibu wake wa kila mwaka kukisaidia chuo hicho.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo jana kwa Shekhe Mkuu wa Mkoa Iringa Abubakar Chalamila, Mchungaji Msigwa alisema kuwa lengo la kugawa kipindi hiki ni kuwaunga mkono Waislamu katika mfungo wa Ramadhani na kuwakumbuka wale wote wanaoishi katika mazingira magumu.
Mchungaji Msigwa alisema ni jukumu la wadau kuweza kuwasaidia wale wote bila kujali itikadi za vyama kwa kuwa binadamu wote ni wamoja kwa sasa.
Mchungaji Msigwa alikabidhi tambi katoni zaidi ya katoni 50, katoni 40 za mafuta ya kupikia, kilo 250 za unga wa ngano na sukari kilo 750 vyote vikiwa na jumla ya thamani zaidi ya shilingi milioni 1.5.
Alisema ataendelea kutoa msaada kwa vituo vingine vya watoto yatima na wasiojiweza katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan.
Akishukuru kwa msaada huo Kwa niaba ya chuo cha Kitanzani Islamic Center chenye jumla ya wanafunzi 120 ambao wanachukua mafunzo ya dini ya kiislamu Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa Iringa, Abubakar Chalamila alisema ni jambo la kujivunia kuwa na mbunge asiyechagua itikadi za dini na mbunge ni akichaguliwa anakuwa wa watu wote bila kubagua watu wake.
“Namshukuru sana Msigwa kwa kuweza kutoa msaada huu na utafikishwa kwa wale wote waliolengwa kupewa na hasa wale wasiojiweza ndio watafaidika na msaada huu wa mbunge wa iringa mjini.” Alisema |Chalamila
Chalamila aliwataka wadau wengine kuwakumbuka watu wasiojiweza na wanaoishi katika mazingira magumu mara kwa mara kwa kuwa ni thawabu kubwa kuweza kuwasaidia.

No comments: