.

JUKATA WACHARUKA SASA WATAKA UKAWA WARUDI BUNGENI MARA MOJA,WASEMA WANANCHI NDIO WANAOTAKA.SOMA HAPA

    
  Na optatucy stan

  Jukwaa la katiba Tanzania JUKATA leo limewasihi wajumbe wa bunge la katiba wanaounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA kurejea katika bunge linalotarajiwa kuanza mapema mwezi kesho kwa kwa masharti ya kufwata rasimu ya katiba mpya iliyopelekwa bungeni na tume ya mabadiliko ya katiba Tanzania.

        Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa jukwaa hilo DEUS KIBAMBA amesema kuwa JUKATA  walifanya utafiti chini ya jopo maalum na kupata nafasi ya kuzungmza na makundi mbalimbali ya wananchi ambao wengi wao waliwataka UKAWA kurejea bungeni kutokana na umuhimu wa bunge hilo kwa watanzania.

  Bw KIBAMBA amesema kuwa jopo hilo limepata nafasi ya kuzungumza na wadau mbalimbali wa kisiasa,asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali ambapo amesema kuwa mengi ya ,makundi hayo yameeleza kuwa kutokana na maslahi ya bunge hilo kwa watanzania kuwa ni makubwa sana wabunge wanaowakilishja umoja wa UKAWA wanapaswa kurudi bungeni ila kwa masharti ya kuendelea na majadiliano ya rasimu ya katiba mpya na si vinginevyo.


     Aidha KIBAMBA ameeleza kuwa mchakato wa uundwaji wa katiba mpya ni jambo la muda mrefu na linahitaji busara ya kutosha hivyo amemtaka spika wa bunge hilo Bw SAMWELI SITTA kuwa kinara wa kutatua tofauti zinapojitokeza kwenye bunge hilo miongoni mwa wabunge.

      Kwa upande wake mkuu wa shule ya sheria ya chuo kikuu cha kenyeta cha nchini kenya Bw PATRICK LUMUMBA amemsihi rais wa Tanzania JAKAYA KIKWETE kuwa na busara katika kipindi hiki cha mabadiliko ya katiba huku akisisitiza kuwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa mataifa mbalimbali hivyo inatakiwa kuonyesha democrasia ya kweli katika mchakato huu,


huku akiwasihi watanzania kuutumia mchakato huu kupata katiba mpya ili kuepuka machafuko kama baadhi ya mataifa ya africa kwa sasa

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.