Tuesday, July 1, 2014

TAARIFA MUHIMU KWA WAISLAM WOTE DAR ES SALAAM--UZINDUZI WA MSIKITI MKUBWA JIJINI IJUMAA YA WIKI HII

Imamu wa msikiti huo SHEKH TWALIB  AHMED ABDALA
akizungumza nasi muda mchache uliopita
         Rais wa awamu ya pili wa Tanzania DK ALLY HASSAN MWINYI anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa msikiti mkubwa na na wa  kihistoria Jijini Dar es salaam siku ya ijumaa tarehe 04 mwezi huu msikiti ambao upo maeneo ya chamanzi mbagala Jijini karibu kabisa na uwanja wa michezo wa azam complex.
      
           Akizungumza na mtandao huu leo jijini Dar es salaam imamu mkuu wa msikiti huo  SHEKH TWALIB AHMED ABDALA amesema kuwa msikiti huo ni mkubwa na una uwezo wa kuchukua takribani watu 800 wakiwemo wanawake na wanaume.

    
      Ufunguzi huo pamoja na swala ya ijumaa utachukua takribani masaa manne ambapo utaanza saa nne  kamili za asubuhi na  kumalizika saa nane kamili mchana ambapo SHEKH TWALIB amewataka waislam wote wa Jiji la Dar es salaam kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo wa kihistoria ukizingatia huu ni mwezi wa ramadhan.

      
 Amesema kuwa katika uzinduzi kutakuwa na mambo mbalimbali kama visomo vya QURUAN,MAWAIDHA NA SALA.

 Msikiti huo wa MASJID HUDDER  unatajwa kuwa ndio msikiti mkubwa Jijini Dar es salaam kwa kuwa na uwezo wa kupokea watu 800 kwa wakati mmoja.

        
 Katika uzinduzi huo utahudhuriwa na viongozi wengine wakubwa wa kiserikali akiwemo makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dk MOHAMED GHALIB BILAL,mke wa rais mama SALMA KIKWETE pamoja na mashekh mbalimbali wa mkoa wa Dar es salaam.


        TUKIO NZIMA LA UZINDUZI HUO TUTAKUWA TUNAKUPA HAPA HAPA.

No comments: