UNAKUMBUKA YALE MABILLION YA USWISI.HUU NDIO MUENDELEZO WAKE

Na Karoli Vinsent
UWEZEKANO wa Mabiloni ya Fedha yaliyofichwa na Vigogo kwenye Mabenki mbalimbali nchini Uswizi,sasa inazidi kuwa  ni ndoto kwa mafedha hayo kurudi kutokana na kutokuwa na nia ya Dhati ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kufanikisha Fedha hizo kurudi nchini,Mtandao huu umebaini.

          Sakata la Mabilioni hayo ya Uswisi yaliibuliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe,ambaye naye kwa sasa ameoneka kama kufungwa mdomo kwenye sakata hilo la kupambana ili fedha hizo ambazo ni chafu ili zirudi nchini.


          Kwa mujibu wa Vyanzo mbalimbali zinasema zaidi ya bilioni 200,zimefichwa na watanzania kwenye Mabenki mbalimbali nchini uswisi,fedha hizo ambazo nyingi zimeonekana kufichwa na viongozi mbalimbali wakiwemo  wabunge,mawaziri wa awamu ya tatu nay a Nne,viongozi wa juu wazamani wa Jeshi, pamoja na wasaka urais ndani CCM,

      Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa Mtandao huu,umebaini hakuna nia ya Dhati iliyofanya na serikali ya Rais kikwete kutokana kupuuza ushauri unaotelewa na watu mbalimbali ambao waliweka mipango ya kuhakisha fedha hizo zinarudi ili zije kuwanufaisha watanzania ambao wnaishi kwenye lindi la umasikini wa kutupwa

           Upuuzi wa kwanza uliofanywa na Serikali ya Rais Kikwete katika sakata hili ni pale ilipokataa ushauri uliotolewa na Jaji mmoja kutoka Ufaransa ,Renaud Van Ruymbele kuhusu hatua ambazo zinatakiwa kufaata ili kuwabaini watu walioficha pesa hizo kwenye Akaunti mbalimbali  za Mapenki huko Uswisi.

          Jaji huyo ambaye anasifika katika Masuala hayo kutokana na Jinsi alivyoweza kuwabaini Akaunt za wafaransi nchini Uswisi ambao walikwepa kulipa kodi.

       Jaji huyo Aliidokeza Serikali ya Tanzania kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Mahesabu ya Serikali (PAC) Zitto Kabwe kwamba taarifa zote kuhusu Watanzania,Alishauri kwanza Serikali ya Tanzania ipeleke Barua ya Maombi kwenye serikali ya Ufaransa ikiwemo wizara ya Sheriaya Ufaransa.
Na endapo Tanzania ikifanya hivyo Kikosi cha kazi kutoka wizara hiyo chini wa jaji huyo wataanza kufuatilia pesa hizo zilizopo nchini uswisi

          Lakini licha ya Serikali ya Tanzania kupewa ushauri huo,lakini kile kinachonekana ni kupuuza ushauri huo,ambao utapeleka pesa hizo kuwa ndoto kulejea kurudi nchini ni kutokana na kitendo alichokifanya wiki iliyopita.

         Mwanasheria Mkuu wa Serikali nchini Fredilick Werema aliponukuliwa na Shirika la Habari la Uingereza(Reuters) akisema kwamba serikali inafuatilia “Suala la urejeshwaji wa Fedha hizo kupitia taasisi moja Binafsi inayoitwa ISCAR iliyopo Basel uswisi ambayo inafanya kazi hiyo ya kurudisha fedha hizo kwa Garama Kamisheni kubwa sana kwa serikali.

         Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa mtandano huu umezidi kugundua ni ndoto fedha kuzidi kurudi kutokana Taasisi hiyo ISCAR iliwai kulalamikiwa na serikali ya Nigeria kwa kufanya kazi kusuasua ,ufuatiliwaji wa Mabilioni yalifichwa na kiongozi Dikteta Sani Abacha.

            Duru za kisiasa zinasema ni ukweli usiopingika kwamba Serikali ya CCM,inazidi kufanya maigizo kwa Watanzania kuhusu suala hili kwani imekosa nia ya Dhati ya kufanikisha pesa hizi nyingi zirudi nchini kutokana na watu wengi walioficha Fedha hizo huku Uswisi kuhusika katika maamuzi mbalimbali ya sheria hapa nchini.  

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.